Mh. John
Malecela.
Ndugu
zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa
kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa
mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo
linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.
Ndugu
waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha
ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa
watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu
cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni
baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana
Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na
baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana
kijana huyu.
Nadiriki
kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa
maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na
watanzania.
Pia
itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu
ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na
kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha mapinduzi (CCM)
kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama
na serikali, nawaomba waendelee -na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi
zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi
wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda
serikali.
Aidha
nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi
cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa
kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu
wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu
la afrika.
Ndugu
zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu
Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu
EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo
la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua
kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi
na katiba -ya chama. Hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya
chama chetu cha mapinduzi iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya?
Je, hapa chama kiko wapi?
Ukweli ni
kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia
tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila
mafanikio.
Naomba
niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao
hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata
madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu
ndani ya chama.
Kinachonisikitisha
zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja
na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu
mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.
Ninaomba
juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama. Ukweli ni kwamba vijana
hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu -kwa
wananchi kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi
bora. Swali: Je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?
Kwa hili
ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri -secretariet ya chama
lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul makonda asingesema haya yote
kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.
Vijana na
wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo
wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya-wengine kupoteza
mwelekeo.
Sisi
tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki
kutumia fedha zake kutaka madaraka. Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za
taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili
ya uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama
sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na
kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni
kwa maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.
Mfano
hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye
vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na
mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.
Mwisho
Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda
na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta
kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.
JOHN
SAMWELI MALECELA
KIDUMU
CHAMA CHA MAPINDUZI
No comments:
Post a Comment