Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo ametoa kauli za uongo kwa nyakati mbalimbali
mwaka 2012 na 2013 ndani na nje ya Bunge kuhusu utafiti na uendelezaji wa gesi
asilia.
Waziri Muhongo alijibu
uongo kwamba hafanyi kazi kwa vyombo vya habari nilipohoji kuhusu utekelezaji
wa maazimio ya Bunge ya kuanzia Novemba 2011 ya kushughulikia ufisadi
uliothibitika katika mapato ya mauzo ya gesi na udhaifu mwingine uliobanishwa.
Aidha, Waziri Muhongo
aliahidi uongo alipounda alipounda kamati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli
(TPDC) na kuahidi kwamba kamati hiyo
itafanya mapitio ya mikataba na kuandaa ripoti itakayowezesha mikataba mibovu
ya utafiti wa mafuta na gesi asili kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, Wizara ya
Nishati na Madini baadaye iliyoa taarifa kwamba matokeo ya ripoti hiyo
hayatatumika kwa ajili ya mikataba iliyopita bali mikataba ijayo.
Pia, Waziri Muhongo
aliahidi kwamba kungekuwa na uwazi kuhusu ripoti hiyo; hata hivyo mara baada ya
kamati kumkabidhi ripoti ameamua kuifanya kuwa sini hata baada ya kuomba kupewa
nakala ya ripoti hiyo kwa mujibu wa masharti ya sheria ya Kinga, Haki na
Madaraka ya Bunge.
Mwaka huu wa 2014
nitatoa kwa umma maelezo ya uongo wa Waziri Muhongo mfululizo kuanzia sasa
mpaka atakapoomba radhi kwa umma na kuchukua hatua zinazostahili kuhakikisha
maslahi ya nchi na matakwa ya wananchi yanazingatiwa kuhusu utafiti na
uendelezaji wa gesi asilia.
Katika kauli itayofuata
nitaeleza uongo wa Waziri Muhongo kuhusu zabuni ya nne ya kunadi vitalu vya
utafiti wa gesi asilia ambao ameueleza kwa nyakati mbalimbali bungeni, katika
Kongamano juu ya Rasilimali lililoandaliwa na UDASA katika Chuo Kikuu cha Dar
Es Salaam na kupitia taarifa kwa umma ilivyotolewa kwenye vyombo vya habari
tarehe 30 Disemba 2014.
lmetolewa na:
John Mnyika (Mb)
6/1/2014
Waziri Kivuli wa
Nishati na Madini
No comments:
Post a Comment