Friday, January 17, 2014
PANGUA PANGUA NIGERIA
Rais Goodluck Jonathan
NIGERIA
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ametangaza kuwa mwenyekiti wa chama tawala cha Peoples Democratic PDP Bw. Bamanga Tukur amejiuzulu.
Rais Jonathan amesema Bw. Turkur hana kosa, na atampatia kazi nyingine muhimu zaidi kuliko ya uenyekiti wa chama cha PDP.
Bw. Bamanga Tukur
Kuanzia mwaka jana chama cha PDP kilikumbwa na changamoto nyingi , viongozi kadhaa wa chama hicho walitaka Bw. Tukur aondolewe madarakani kwa kuwa hakuchukua hatua zenye ufanisi kukabiliana na changamoto hizo.
Habari nyingine kutoka ikulu ya Nigeria zinasema, mkuu wa jeshi la ulinzi la Nigeria Jenerlai Ola Ibrahim ameondolewa madarakani, na nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa mkuu wa jeshi la anga Alex Bad.
Ola Ibrahim
Msemaji wa ikulu ya Nigeria amesema mbali na Jenerali Ola Ibrahim, wakuu wa majeshi ya majini, anga na ardhini pia watabadilishwa.
Taarifa haijaeleza sababu za mabadiliko hayo, lakini watu wanahisi hatua hiyo huenda ni kutokana na kuboresha hali ya usalama nchini Nigeria na kuimarisha nguvu za kupambana na kundi la Boko Haram.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment