Mwanamitindo
anayefanya vizuri sana nchini, Danny David atazindua kampuni yake mpya ya
Gracing Africa inayojihusisha na ukuzaji na uendelezaji wa vipaji nchini hasa
vya mitindo na fashion ijumaa hii katika hoteli ya Serena ambapo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa meya wa jiji la Dar es Salaam mheshimiwa Jerry Slaa.
Uzinduzi
huo wa aina yake utakuwa wa mwaliko pekee ni watu wachache watakaochaguliwa
kuhudhuria sherehe hiyo.
Danny
ambaye hivi karibuni amerejea nchini toka nchini Afrika ya kusini alipoenda kwa
ajili ya shuguli za kizazi amesema lengo la kampuni hiyo ni kukuza na
kuendeleza vipaji vya vijana wengi nchini katika lengo la kuboresha maisha yao.
No comments:
Post a Comment