KIUNGO WA KIMATAIFA WA HISPANIA NA KLABU YA BARCELONA XAVI
HERNANDEZ HAPO JANA ALICHEZA MECHI YAKE YA MIA SABA AKIWA NA BARCELONA IKIWA
IMEPITA MIAKA 16 TANGU ALIPOCHEZA MECHI YAKE YA KWANZA NDANI YA KLABU HIYO .
XAVI HERNANDEZ AMEICHEZEA BARCELONA KWA MAFANIKIO MAKUBWA HADI
KUFIKIA HADHI YA KUTAMBULIKA KAMA MOJA YA VIUNGO BORA WALIOWAHI KUTOKEA DUNIANI
AKIWA AMEIONGOZA KLABU HIYO KUTWAA MATAJI 19 KATIKA KIPINDI CHOTE ALICHOCHEZA.
KATIKA MCHEZO WA JANA WA KOMBE LA HISPANIA FC BARCELONA
ILISHINDA KWA MABAO MAWILI BILA , MABAO YOTE YAKIFUNGWA NA LIONEL MESSI.
LAKINI PIA KIUNGO WA MANCHESTER UNITED M-BRAZIL ANDERSON
AMEJIUNGA NA KLABU YA FIORENTINA KWA MKOPO MPAKA MWISHONI MWA MSIMU.
ANDERSON AMBAYE ANA UMRI WA MIAKA 25 AMEKUWA NJE YA KIKOSI CHA
KWANZA CHA MAN UNITED KWA MUDA MREFU KIASI CHA KUTOKUWA SEHEMU YA MIPANGO YA
BAADAYE YA KOCHA DAVID MOYES NA FIORENTINA INAYOSHIRIKI LIGI YA ITALIA ITAMPA
KIUNGO HUYO NAFASI YA KUPATA MECHI MFULULIZO HALI INAYOTARAJIWA KUREJESHA
KIWANGO CHAKE .
ENDAPO KLABU HIZO MBILI ZITAFIKIA MAKUBALIANO , ANDERSON HUENDA
AKAJIUNGA NA FIORENTINA MOJA KWA MOJA KWA ADA YA UHAMISHO YA PAUNDI MILIONI 6.5.
NAYE KOCHA WA REAL MADRID CARLO ANSHELOTI AMEKIRI KUWA KLABU
YAKE ILIFANYA MAKOSA KUMRUHUSU KIUNGO WA KIMATAIFA WA UJERUMANI MESUT OZIL
KUIHAMA KLABU HIYO NA KUJIUNGA NA ARSENAL.
OZIL AMBAYE KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE ALIYOKUWA REAL MADRID
ALIKUWA ANAONGOZA KWA KUTENGENEZA NAFASI ZA KUFUNGA KWA WENZIE ALIIHAMA MADRID
MWANZONI MWA MSIMU HUU NA KUSAJILIWA NA ARSENAL KWA BEI YA PAINDI MILIONI 42.5
HUKU AKICHA MALALAMIKO KWA WACHEZAJI WENZIE A NDANI YA KIKOSI CHA REAL MBAO
HAWAKUFURAHISHWA NA KITENDO CHA MADRID
KUMUACHIA .
MMOJA WA WATU AMBAO WALIKERWA SANA NA KUONDOKA KWA OZIL ALIKUWA
MCHEZAJI BORA WA DUNIA CRISTIANO RONALDO AMBAYE ALIDAI KUWA OZIL ALIKUWA
AKIMSAIDIA SANA KWENYE UFUNGAJI WA MABAO KUTOKANA NA UMAHIRI WAKE KWENYE KUPIGA
PASI ZA MWISHO
NA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU NCHINI MAREKANI NBA IMEZINDUA RASMI
JEZI ZITAKAZOVALIWA KWENYE MICHEZO YA WACHEZAJI NYOTA YAANI NBA ALL STARS .
JEZI HIZO KWA MSIMU WA MWAKA HUU ZITAKUWA NA MABADILIKO AMBAPO
ZIMEBUNIWA KWA MTINDO WA FULANA ZA KAWAIDA ZENYE MIKONO MIREFU NA SIO ZILE
AMBAZO HAZINA MIKONO ZILIZOELEKA.
NBA ALL STARS NI UTAMADUNIA WA LIGI YA NBA KUWAKUTANISHA
WACHEZAJI NYOTA KATIKA MFULULIZO WA MICHEZO NA MASHINDANO TOFAUTI NA MWAKA HUU
MICHEZO HIYO ITAFANYIKA HUKO NEW OLINS AMBAKO TIMU MWENYEJI ITAKUWA THE NEW
OLINS PELICANS .
No comments:
Post a Comment