“Baba Na mengi ya
kukueleza Baba, niseme Kitu gani ujue ninakupenda baba, niseme nini ujue
ninakuthamini Baba, niongee lugha gani ujue ninakujali Baba, nikulipe nini ujue
ninakushukuru Baba, Sina cha kukulipa Baba, ila nakuombea maisha marefu Baba,
Mbona Una roho ya pekee Baba, Mbona uko tofauti Na wengine Baba, nashukuru kwa
kunisitiri Baba, nashukuru kwa kunijali Baba, nashukuru kwa kunitoa shimoni
Baba, Baba Sina cha kukulipa Baba,ila nakuombea maisha marefu Baba,walinikimbia
wengi nilipopata matatizo Baba ,lakini Baba yangu huku niacha nife Baba, Baba
ulihangaika kuokoa uhai wangu Baba, Huruma yako ndio ilioniokoa Baba, Bila wewe
Baba Leo ningeitwa Marehemu Baba, nikulipe nini Baba????
Sina cha kukulipa Baba
ila nakuombea afya njema Na maisha marefu Baba, roho yako ni ya kipekee
Baba,Mungu akulinde Baba,M ungu akupe maisha marefu Baba,Bila wewe Baba, Leo
nisingekuwa nilipo Baba,Nathamini Msaada wako Baba, Na ninahaidi Kamwe
sitakuangusha Baba, umenifanya Nijithamini Na kujijali Baba, umenifanya
nijijali Baba, umenipa Nguvu ya kusimama mbele ya watanzania wenzangu Na
kuwaelezea madhara ya madawa ya kulevya Baba, Leo hii nasimama kupiga vita
dhidi ya madawa ya kulevya Baba…..Umenipa ujasiri wa ajabu Baba, Sina cha
Kukulipa Baba Ila Mungu Atakulipa Baba…..Tanzania Bila Madawa ya Kulevya
Inawezekana……Happy New Year Dad………#Myhero#Mydad#Mypresident#Amen”
No comments:
Post a Comment