NCHINI HISPANIA ATLETICO MADRID WALIPATA FURSA ADIMU YA KUONGOZA
LIGI WALAU KWA SAA 24 KUFUATIA USHINDI KIDUCHU WALIOUPATA KWENYE MCHEZO WAO
DHIDI YA MALAGA ULIOPIGWA JUMAMOSI .
KATIKA MCHEZO HUO ATLETICO WALISHINDA KWA BAO MOJA BILA MFUNGAJI
AKIWA MCHEZAJI ANAYEWANIWA NA MANCHESTER UNITED KOKE .
MABINGWA WATETEZI WA LIGI YA HISPANIA FC BARCELONA WALIRUDI
KWENYE KITI CHAO JUMAPILI BAADA YA KUWAFUNGA ELCHE MABAO MANNE BILA .
WAFUNGAJI WA BARCA WALIKUWA ALEXIS SANCHEZ AMBAYE ALIFUNGA MABAO
MATATU NA PEDRO RODRIGUEZ .
KWENYE LIGI YA ITALIA MABINGWA WATETEZI JUVENTUS WALIENDELEA
KUKALIA KITI CHA UONGOZI WA LIGI HIYO BAADA YA KUWAFUNGA AS ROMA KWA MABAO
MATATU BILA .
WAFUNGAJI WA JUVENTUS WALIKUWA ARTURO VIDAL , LEORNADO BONUCHI
NA MIRKO VUCHINICH.
KATIKA MCHEZO MWINGINE WA LIGI YA ITALIA ULIOPIGWA JANA ,
FIORENTINA
WALIWAFUNGA LIVORNO KWA BAO MOJA BILA .
MFUNGAJI WA BAO HILO ALIKUWA GONZALO HAVIER RODRIGEZ
WAKATI LIGI NYINGI ZIKIWA ZINARUDI BAADA YA KUSIMAMA KUPISHA
MAPUMZIKO YA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA LIGI YA ENGLAND ILISIMAMA
KUPISHA MICHUANO YA KOMBE LA FA AMBAYO ILIKUWA INACHEZA KWENYE RAUNDI YAKE YA
TATU.
KATIKA MICHEZO ILIYOPIGWA JUMAMOSI ARSENAL THE GUNNERS
WALIWAFUNGA WAPINZANI WAO WA JADI AMBAO PIA NI JIRANI ZAO KWENYE MAENEO YA
KASKAZINI MWA JIJI LA LONDON TOTTENHAM HOTSPURS .
KATIKA MCHEZO HUO ARSENAL WALISHINDA KWA MABAO MAWILI BILA ,
MABAO YALIYOFUNGWA NA SANTIAGO CATHOLA, TOMAS ROZISKI .
KATIKA MCHEZO MWINGINE MANCHESTER CITY WALIBANWA MBAVU KWA
KULAZIMISHWA SARE YA BAO MOJA KWA MOJA NA TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA
BLACKBURN ROVERS .
CITY WALIANZA KUFUNGA KUPITIA KWA ALVARO NEGREDO KABLA YA SCOTT
DUNN HAJAISAWAZISHIA ROVERS KATIKA MCHEZO ULIOPIGWA HUKO EWOOD PARK . TIMU HIZI
ZITARUDIANA KWENYE UWANJA WA MAN CITY ETIHAD STADIUM TAREHE KUMI NA NNE YA
MWEZI HUU.
KATIKA MICHEZO ILIYOPIGWA JUMAPILI TIMU YA LIGI KUU YA ENGLAND
YA WEST HAM UNITED ILIPATA AIBU YA KUANZIA MWAKA BAADA YA KUTOLEWA MASHINDANONI
KWA KIPIGO CHA HISTORIA CHA MABAO MATANO BILA TOKA KWA NOTTINGHAM FOREST ,
WAFUNGAJI WA FORREST WALIKUWA DJAMEL ABDOUN , ANDY REID PAMOJA
NA JAMIE PATTERSON AMBAYE ALIFUNGA MABAO MATATU.
NAO CHELSEA WALIWAFUNGA DERBY COUNTY KWA MABAO MAWILI BILA .
MABAO YOTE MAWILI YALIFUNGWA NA VIUNGO LA KWANZA LIKIFUNGWA NA
MNIGERIA JOHN OBI MIKEL NA LA PILI LIKIFUNGWA NA MBRRAZIL OSCAR.
MWANZO MBAYA WA MWAKA ULIENDELEA KWA MANCHESTER UNITED YA DAVID
MOYES AMBAYE KWA MARA YA PILI MFULULIZO ILIKUBALI KIPIGO KWENYE UWANJA WAKE WA
NYUMBANI OLD TRAFFORD AMBAKO WALIFUNGWA MABAO MAWILI BILA NA SWANSEA CITY .
SWANSEA WALIFUNGA KUPITIA KWA WAYNE RAUT-LEJ NA WILFRED BONI
HUKU UNITED WAKIFUNGA KUPITIA KWA HAVIER HENANDEZ CHICHA-RITO.
ANGA LA SOKA LIMEANZA WIKI YA PILI YA MWAKA MPYA WA 2014 KWA
SIMANZI KUU KUFUATIA TAARIFA ZA KIFO CHA GWIJI WA ZAMANI WA URENO USEBIO DA
SILVA FERREIRA ALIYEFARIKI DUNIA ASUBUHI YA JUMAPILI TAREHE TANO MWEZI HUU.
EUSEBIO AMBAYE ANA ASILI YA BARA LA AFRIKA AKIWA AMEZALIWA
NCHINI MSUMBIJI KABLA YA KUHAMIA BARANI ULAYA ALIKOPEWA URAIA WA URENO ANA
SEHEMU YAKE KATIKA HISTORIA YA SOKA HUSUSAN NCHINI URENO ANAKOTAZAMWA KAMA
MMOJA WA WACHEZAJI BORA WA MUDA WOTE KATIKA HISTORIA YA TAIFA HILO.
DUNIA ITAMKUMBUKA USEBIO KWA MABAO YAKE TISA ALIYOFUNGA KWENYE
KOMBE LA DUNIA MWAKA 1966 HUKO NCHINI ENGLAND AMBAKO TIMU YAKE YA TAIFA YA
URENO ILIFIKIA HATUA YA NUSU FAINALI AMBAPO ALIMALIZA MICHUANO HIYO AKIWA
MFUNGAJI BORA .
AKIWA NA KLABU YA BENFICA , USEBIO ALITWAA UBINGWA WA ULAYA MARA
MOJA , SAMBAMBA NA MATAJI MATANO YA UBINGWA WA KOMBE LA URENO NA UBINGWA WA
LIGI AMBAO ALIUTWAA MARA 11.
USEBIO PIA ALITUNUKIWA TUZO KADHAA KUTOKANA NA UBORA WAKE KAMA
MCHEZAJI BINAFSI AMBAPO ALIWAHI KUWA MCHEZAJI BORA WA URENO MARA MBILI ,
MCHEZAJI BORA WA ULAYA MARA MOJA , PAMOJA NA TUZO TATU ZA UFUNGAJI BORA BARANI
ULAYA PEMBENI YA ILE YA UFUNGAJI BORA WA KOMBE LA DUNIA .
SIFA KUBWA YA USEBIO UWANJANI ILIKUWA NI NGUVU HALISI ALIZOKUWA
NAZO HASA MIGUUNI KWAKE AMBAKO ALISIFIKA SANA KWA MASHUTI MAKALI ALIYOKUWA
AKIPIGA PAMOJA NA KASI AMBAYO ILIMFANYA KUUCHEZEA MPIRA KWA WEPESI ULIOWAPA
TABU MABEKI ALIOKUWA AKIKUMBANA NAO NA
HAISHANGAZI KUONA TAKWIMU ZINAZOONYESHA
KUWA ALIFUNGA MABAO MIA SABA ISHIRINI NA SABA KATIKA MICHEZO MIA SABA KUMI NA
TANO , KWA MAHESABU YA HARAKA USEBIO ALIKUWA AKIFUNGA WALAU BAO MOJA KWENYE
KARIBU KILA MECHI ALIYOCHEZA.
MWEZI JANUARI NI MWEZI AMBAO UNA MAANA KUBWA KWENYE HISTORIA YA GWIJI HUYU MRENO MWENYE DAMU YA
KIMAKONDE , ALIZALIWA TAREHE 25 JANUARI MWAKA 1942 NA ALIFARIKI DUNIA TAREHE
TANO JANUARI MWAKA 2014 SIKU 20 TU KABLA YA KUSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA
BAADA YA KUPAMBANA KWA MUDA MREFU NA MARADHI YA MOYO NA KIHARUSI , REST IN
PEACE , EUSEBIO DA SILVA FERREIRA.
No comments:
Post a Comment