Nyota wa Chelsea Frank Lampard na Branislav
Ivanovic watakuwa nje kwa Mwezi
mmoja baada kuumia kwenye Mechi na Liverpool
ambayo walishinda 2-1 Uwanjani
Stamford Bridge hivi Juzi. Habari hizi pia
zimethibitishwa na Meneja wa
Chelsea Jose Mourinho akiongea mara baada ya
kuichapa Southampton 3-0 Siku ya Mwaka
mpya.Ivanovic, mwenye Miaka 29 na anaetoka Serbia,
ameumia Goti na Lampard, Miaka 35,
ameumia Musuli. Lampard, Msimu huu,
amefunga Bao 4 katika Mechi 18 za Ligi na Ivanovic amechezeaMechi zote 26 za
Chelsea katika Mashindano yote Msimu huu.
No comments:
Post a Comment