Michael Schumacher alinuia kuadhimisha miaka 45 ya
kuzaliwa kwake akiwa na jamaa na marafiki zake wa karibu, akiwa katika
mapumziko ya msimu wa baridi nchini Ufaransa, lakini mambo hayakwenda hivyo.
Siku tano baada ya kupata ajali mbaya wakati akishiriki
mchezo wa kuteleza juu ya barafu, shujaa huyo aliyestaafu kutoka mbio za magari
ya Formula One bado yuko katika hali mbaya hospitalini ijapokuwa madaktari
wanasema wameidhibiti hali yake.
Ajali ya Schumacher imevigonga vichwa vya habari kote
ulimwenguni, huku ujumbe ukiendelea kumiminika kutoka kila pembe wa kumtakia
ahueni ya haraka. Schumacher bado yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Na kama hatua ya kuonyesha mshikamano na familia ya
bingwa huyo wa Formula One, mashabiki wamekesha usiku kucha, wakimwombea
Schumi. Kampuni aliyoihudumia ya Ferrari, iliwasafirisha mashabiki kwa mabasi
kutoka Italia hadi mjini Grenoble, kusini mashariki ya Ufaransa, ili kumwombea
shujaa wao. Nami hapa kwa niaba ya jamii ya DW tunajiunga na ulimwengu katika
kumtakia shujaa huyo ahueni ya haraka
No comments:
Post a Comment