Mapema, wakurugenzi wa
sekta ya madini katika Serikali za Tanzania na Finland, walitiliana saini ya
kukuza na kuendeleza sekta ya madini hapa nchini.
Dar es Salaam. Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo, amejigamba kuwa Tanzania
haitadanganyika tena kwa wawekezaji wa sekta ya madini kutolipa kodi na
kuifanya nchi kutofaidika na rasilimali zake.
Alisema hayo juzi
katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya Serikali za Tanzania na
Finland, kutiliana saini, makubaliano katika kutafiti na kukuza sekta ya
madini.
“Kama ni kutuibia
walifanya hivyo siku za nyuma, lakini kwa sasa hawawezi tena,” alijigamba
Profesa Muhongo akidai historia inaonyesha kuwa nchi zote zenye rasilimali za
madini, mwanzoni zilidanganyika.
Alikiri kuwa awali
wawekezaji katika migodi walikuwa wakijitetea kuwa walikuwa wanapata hasara
lakini kwa sasa, sheria inawalazimisha kulipa asilimia 30.
Kauli ya Profesa
Muhongo ilitokana na waandishi kumbana, kuhusu Watanzania kutonufaika na sekta
ya madini wakati ina faida kubwa.
Profesa Muhongo alisema
kwa sasa sekta ya madini inachangia asilimia 3.5 ya pato la Taifa.
Alisema malengo ni
kuhakikisha kuwa sekta ya madini inachangia zaidi ya asilimia 10 ifikapo mwaka
2025.
Mapema, wakurugenzi wa
sekta ya madini katika Serikali za Tanzania na Finland, walitiliana saini ya
kukuza na kuendeleza sekta ya madini hapa nchini.
Akizungumzia
makubaliano hayo, Profesa Muhongo alisema yanazingatia mambo matatu, ambayo ni
pamoja na utafiti wa madini katika mikoa ya kusini.
Alisema kimsingi tayari
wamegundua kuwa ukanda huo una makaa ya mawe, shaba, niko na platiniamu.
Alisema
watakachokifanya ni kuainisha maeneo yenye madini na viwango halisi ili
wakipatikana wawekezaji wa kuyachimba, waingie kwenye makubaliano ya uhakika.
No comments:
Post a Comment