Wednesday, January 15, 2014

HILI NDILO DAMPO JIPYA NA LA KISASA LA KUTUPIA TAKATAKA LINALO JENGWA JIJINI MBEYA.


Huu ndio mwonekano wa Dampo hilo la kisasa kwa upande wa juu ambapo ujenzi upo katika hatua za mwishoni 

 Hili ni eneo ambapo magari yaliyobeba takataka yatakua yanaingia na kumwanga taka taka hizo 

 Mwonekano wa Karibu wa ndani wa Dampo hilo la kisasa Jijini Mbeya 
 Hii ni Chemba pekee ambayo ni maalum kwa ajili ya kupitishia takataka zenye kimiminika, pia kupitishia takataka ambazo zitakuwa zimesagwa na kupelekwa katika Bwawa maalum litakalo tumika kutengenezea umeme pamoja na mabaki mengine ya takataka yatatumika kutengenezea mbolea 
 Hapa Ndipo Takataka hizo zitakuwa zikiteremkia 
 Mwonekano zaidi wa Dampo hilo la kisasa kwa ndani ambapo kwa sasa wameweka kokoto ndogondogo chini  huku ujenzi ukiendelea 

 Kingo pembezoni mwa Dampo hilo la kisasa 

 Hii ni sehemu maalum ambayo itajengwa kisasa kwa ajili ya kuoshea magari baada ya kumwaga takataka 
Hii ni sehemu ya kupaki magari ambayo yatakuwa yakitupa takataka katika dampo hilo la kisasa 

HIVI NDIVYO TAKATAKA ZILIVYOKUWA ZIKITUPWA KABLA YA DAMPO HILO KUJENGWA KATIKA ENEO HILO.


Pichani ni jinsi takataka kutoka pande mbalimbali za jiji la Mbeya zilivyokuwa zikitupwa kabla ya Dampo hilo la kisasa kujengwa katika eneo hilo jirani na Mlima Nyoka Jijini Mbeya.

Dampo hilo la kisasa linategemea kuanza kufanya kazi hivi karibuni

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG.

No comments:

Post a Comment