Mshindi wa taji la
urembo wa Venezuela mwaka 2004 (Miss Venezuela 2004) Monica Spear ameuawa kwa
kupigwa risasi na majambazi jumatatu, January 6.
Kwa mujibu wa The
Associated Press, Majambazi hao pia walimuua kwa risasi mumewe Henry Thomas
Berry aliyekuwa naye kwenye gari, na kumjeruhi mguuni mtoto wao wa kike mwenye
umri wa miaka 5
miss monica spear akiwa
na mpenzi wake henry thomas enzi za uhai wao
Majambazi hao walianza
kufyatua risasi. Director wa upelelezi wa Polisi wa Venezuela, Jose Gregorio
amesema takribani risasi sita zilifyatuliwa na majambazi hao, na kwamba mtoto
Maya anaendelea vizuri na matibabu.
Monica Spear aliwahi
kuzing’arisha tamthilia nyingi ikiwa ni pamoja na tamthilia maarufu ya ‘Pasion
Prohibida’
Gari ambalo
walikuwemo wakati wa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment