Tuesday, December 24, 2013

HAFLA FUPI YA SHIRIKISHO LA NGUMI ZA RIDHAA TANZANIA KWA AJILI YA KUHAMASISHA MCHEZO WA NGUMI KWA VIJANA TANZANIA.


 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa wa ngumi za Ridhaa pamoja na wadau wengine wa mchezo huo katika Picha ya pamoja, wakati wa hafra hiyo
 Aliyesimama kushoto ni mkurugenzi wa Afrika Mashariki kupitia kinywaji cha Battery Bwana Tony Misokia akiwa anaongea na wananchi walioshiriki katika Hafra hiyo.
 
 Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF) Bwana. Lukelo  Anderson akiwa sambamba na Afisa habari wa Ngumi za ridhaa Tanzania  Bwana Salum Viduka wakati wa Hafra hiyo.

 Hawa ni Baadhi ya wachezaji wa  Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF)

 Wa kwanza kulia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi za ridhaa Tanzania bwana Nassari Mafuru
 Kutoka kushoto aliyevaa shati jeupe ni Bwana Anthon Mwang'onda ambaye ni mjumbe wa mashindano na vifaa wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF) akiwa na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Bwana Hassan Mzonge


*******

Shirikisho la ngumi za ridhaa Tanzania  limefanya hafra fupi iliyo jumiisha wachezaji wa ndondi , makocha wadau na Vyombo vya habari kwaajiri ya kuendeleza kuweka mshikamano wa kuweza kuwainua vijana ambao bado hawajaweza kupata ajira  kuweza kujiunga na shilikisho la ngumi za ridhaa Tanzania

Shilikisho hilo ambalo limeanzisha mashindano ambayo yanatambulika kwa jina la  PSPF  Boxing Award sambamba na waandaaji wa Hafla hiyo wakiwa ni wadhamini wa mashindano hayo  iliyofanyika katika eneo la   (CnG) ambapo waliweza kudhamini kwa kuandaa chakula cha usiku kwaajili ya kuendelea kuweka mahusiano baina ya washiriki wote wanao shiriki katika kuendeleza mchezo wa ngumi Tanzania

Akizungumzia lengo la kuweka hafra  hiyo Afisa habari wa shirikisho la ngumi Tanzania Bw.Salum Kuhowa Viduka amesema "Tunawaomba wanajamii kuweza kutupa ushirikiano kwa muda wote ambao mashindano haya yanapo kuwa yana wasili katika miji,wilaya,manispaa,na nk kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuona jinsi fursa kwa vijana zinavyo patikana kupitia mchezo wa ngumi za Ridhaa"

Mwisho Makamu Rais  Bw.Lukelo Andason aliweza kufunga hafla hiyo kwa kuwapongeza watu wote walio weza kufika na kujumuika pamoja ili kuendeleza kujenga umoja wa ngumi Tanzania
 



No comments:

Post a Comment