“Waziri
hana mamlaka ya kumwondoa mkurugenzi wa halmashauri, taasisi, shirika na katibu
wa wizara yake kutokana na kubanwa na mfumo.” Makamba.
Mwanza.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba amesema ipo haja ya kubadili mfumo wa watendaji
serikalini ili wanapoboronga nao wajibishwe na mawaziri.
Akizungumza katika
mahojiano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini hapa, Makamba alisema mfumo
uliopo sasa, hauwapi nguvu mawaziri ili
kuwawajibisha watendaji pale wanapokosea na badala yake unawabana wenyewe hivyo
kuendelea kuwa kitanzi kwao.
“Mimi ni waziri,
akikosea katibu nawajibishwa huyu anabaki, mimi siwezi kumwajibisha hivyo
wanafanya lolote na sisi tunalazimishwa kuwajibishwa kisiasa kwa makosa ya
watendaji,” alisema.
“Baada ya Kamati ya
Maliasili Ardhi na Mazingira iliyo chini ya Mwenyekiti wake, James Lembeli
kuomba kwa Spika kutumia ushahidi kwa kuweka kanda za video ili kuonyesha
kilichotokea kwenye Operesheni Tokomeza Ujangili, hali ilichafuka ndani ya
kikao cha Bunge na kila mmoja akawa na hisia na wengine kuanza kububujikwa na
machozi na wabunge kuchangia hoja za kutaka mawaziri kuachia ngazi,
hawakuangalia kiini cha tatizo, waliwabana mawaziri tu,” alisema.
Alisema Serikali
kupitia mamlaka za juu, inapaswa kuangalia mfumo uliopo kwa lengo la
kuubadilisha na kuingiza mapendekezo na mfumo mpya kwenye Katiba Mpya kuhusu
uwajibikaji wa mawaziri na watendaji wakuu kwenye wizara, taasisi, idara,
halmashauri na mashirika ya umma ambao ni wataalamu mbalimbali kuwajibishwa na
mawaziri husika endapo kutaonekana utendaji wao haukidhi ama kwenda kinyume na
maadili na sheria zilizopo.
No comments:
Post a Comment