Thamsanqa Jantjie,
mkalimani wa lugha ya ishara
Mkalimani wa lugha ya
ishara katika siku ya mazishi ya kitaifa, ya aliyekuwa rais wa kwanza mzalendo
wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa katika hospitali ya magonjwa ya
akili.
Mkalimani huyo
anashutumiwa kutoa ishara ambazo hazikuendana na kile kilichokuwa kikiongelewa.
Thamsanqa Jantjie
"anaweza kuwa na matatizo", amekaririwa mke wake Siziwe akisema hayo.
Wataalam wa lugha ya ishara
wamemshutumu kwa kutoa tafsiri potofu wakati viongozi mbalimbali wakitoa hotuba
zao kwenye mazishi ya kitaifa ya Bwana Nelson Mandela wiki iliyopita.
Bwana Jantjie amesema
aliumwa ghafla ugonjwa wa schizophrenia.
Amesisitiza kuwa
alikuwa ni mkalimani mwenye ujuzi wa kazi hiyo.
Chama tawala cha
African National Congress,ANC, amesema imekuwa ikimtumia Bwana Jantjie kama
mkalimani wa lugha ya ishara katika matukio kadha siku za nyuma na hakuwahi
kulalamikiwa kuhusiana na huduma yake, kwa upande wa ujuzi au maradhi yoyote.
Bwana Mandela alifariki
dunia tarehe 5 Desemba mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95 na kuzikwa Jumapili.
No comments:
Post a Comment