Tuesday, December 10, 2013

MSONDO, SIKINDE KUPAMBANA KRISMASI TCC CLUB CHANG’OMBE


Msondo
Sikinde




Wafalme wa muziki wa dansi nchini bendi pizani za Msondo Ngoma “Baba ya Nuziki’ na Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae)  watapambana siku ya Krismasi katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.

Mpambano huo umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na Konyagi na Nipashe.

Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2013.

Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani bora ya mwaka huu.

Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa. Kila bendi itapiga muziki jukwaani kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda.

“Litakuwa ni pambano la aina yake ukizingatia kila bendi ina vyombo vipya walivyopewa na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (Konyagi). Pia tutakuwa na michezo aina mbalimbali ya watoto,” alisema Kapinga.

Alisema mchuano huo utaanza saa nane mchana hadi majogoo.

Wadhamini wengine wa shindano hilo ni pamoja na gazeti la Nipashe, Saluti5 na CXC Africa

No comments:

Post a Comment