Timu ya taifa ya
Tanzania
Timu ya taifa ya
Tanzania bara "Kilimanjaro Stars" imesonga mbele hatua ya robo
fainali ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA
Senior Challenge baada ya kuisambatisha timu ya Taifa ya Burundi "Intamba
mu Rugamba" kwa goli 1 - 0.
Goli la Tanzania
limefungwa dakika ya 8 kipindi cha kwanza na Mbwana Samatta mshambuliaji wa
timu hiyo anachezea Klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kwa matokeo hayo ya
mchezo huo wa kundi A unaifanya Tanzania bara sasa kufikisha pointi 7 baada ya
kushinda mechi mbili na kutoka sare mmoja.
Tanzania ilitoka sare
na Zambia ya goli 1 - 1 katika mchezo wa ufunguzi siku ya Alhamis iliyopita
ambapo baadae iliifunga Somalia goli 1 - 0 mechi iliyopigwa siku ya jumapili
kabla ya kushinda mechi kati yake na Burundi ya goli 1 - 0.
Katika mchezo mwingine
wa kundi A Zambia walitarajiwa kupambana na Somalia.
No comments:
Post a Comment