Polisi ya Kenya siku ya
Jumapili (tarehe 15 Desemba) ilimtia mbaroni mtuhumiwa mmoja kuhusiana na
mlipuko ndani ya basi katika eneo la Pangani jijini Nairobi ambao uliua watu
sita na kujeruhi wengine wapatao 30, AFP iliripoti.
Mkuu wa Polisi wa
Nairobi Benson Kibue alisema kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa akihojiwa juu ya
shambulio la Jumamosi kwenye basi la watu 32 ambalo sehemu yake ya nyuma
iling'olewa kwa mlipuko huo.
"Tumemshikilia
mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa mara tu baada ya tukio. Anatusaidia katika
uchunguzi," Kibue alisema, na kutoa tahadhari kamba ilikuwa mapema sana
kusema iwapo mtu huyo "alihusika moja kwa moja katika shambulio".
Waranti pia ilikuwa
imetolewa kwa kumkamata mtuhumiwa wa pili, mwenye umri wa miaka 21, Hussein Nur
Mohamed. Polisi walichapisha picha ya Mohamed na kutoa wito kwa wananchi
kujitokeza wakiwa na habari yoyote ile.
Polisi wanafanyakazi
kuamua iwapo mripuko huo uliokuwa wa nguvu kubwa ulisababishwa na guruneti au
chombo cha mlipuko cha kutengeneza, na iwapo chombo hicho kilikuwa ndani ya
basi, kikiwa kimechukuliwa na abiria au kilirushwa kutoka nje.
Mlipuko huo ulizipiga
gari kadhaa karibu na basi, na kuua angalau mwendesha pikipiki mmoja, kwa
mujibu wa mashuhuda.
Lilikuwa shambulio la
nne ndani ya wiki ambayo Kenya iliadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kutoka
Uingereza, ikiwa ni pamoja na jaribio la shambulio kwa watalii wa Kiingereza
huko Mombasa na shambulio kwa polisi wa Kenya karibu na mpaka wa kaskazini
mashariki na Somalia.
Ijumaa iliyopita, siyo
chini ya mtu mmoja aliuawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya sana wakati
milipuko miwili kuutikisa mji wa Wajir kwa wakati mmoja, polisi walisema, jambo
linaloashiria kwamba ilionekana kama kazi ya wapiganaji wa al-Shabaab au
wafuasi wao.
Hakuna mahusiano
yaliyowekwa baina ya mashambulio hayo, ambao hakuna kikundi chochote kilichodai
kuhusika.
Siku ya Jumamosi, hali
ilikuwa shwari huko Eastleigh baada ya polisi siku ya Jumamosi jioni kuwatawanya
watu waliokuwa wanafanya fujo katika mtaa ambako mlipuko huo ulitokea.
No comments:
Post a Comment