LIGI KUU YA ENGLAND IMEENDELEA MWISHONI MWA WIKI HII KWA MICHEZO
KADHAA ILIYOKUJA NA MATOKEO YA KUSISIMUA .
JIJINI MANCHESTER KWENYE UWANJA WA ETIHAD WENYEJI MANCHESTER
CITY WALIENDELEZA REKODI YAO NZURI KWENYE UWANJA WA NYUMBANI BAADA YA KUWAFUNGA
ARSENAL KWA MABAO SITA KWA MATATU .
WAFUNGAJI WA MAN CITY WALIKUWA FERNANDINYO AMBAYE ALIFUNGA MABAO
MAWILI , YAYA TOURE , DAVID SILVA , SERGIO AGUERRO NA ALVARO NEGREDO HUKU
ARSENAL WAKIFUNGA KUPITIA KWA THEO WALCOTT AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI NA PER
METERSECKER .
KATIKA MCHEZO MWINGINE ULIOPIGWA JUMAMOSI CHELSEA WALIWAFUNGA
CRYSTAL PALACE MABAO MAWILI KWA MOJA .
WAFUNGAJI WA CHELSEA WALIKUWA FERNANDO TORRES NA RAMIRES HUKU
CRYSTAL PALACE WAKIFUNGA KUPITIA KWA MARUAN SHAMAK.
KATIKA MICHEZO ILIYOPIGWA JUMAPILI MANCHESTER UNITED WALISHINDA
KWA MARA YA KWANZA BAADA YA MICHEZO MINNE BAADA YA KUWAFUNGA ASTON VILLA MABAO
MATATU BILA .
WAFUNGAJI WA UNITED
WALIKUWA DANNY WELBECK AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI NA TOM CLEVERLEY.
NAO LIVERPOOL WAKIWA UGENINI WALIWAFUNGA TOTTENHAM HOTSPURS
MABAO MATANO BILA .
WAFUNGAJI WA LIVERPOOL WALIKUWA LUIS SUAREZ AMBAYE ALIFUNGA
MABAO MAWILI , JORDAN HENDERSON , JOHN FLANAGAN NA RAHEEM STERLING.
NCHINI HISPANIA KLABU YA REAL MADRID ILIBANWA SIKU YA JUMAMOSI
BAADA YA KULAZIMISHWA SARE NA OSASUNA KATIKA MCHEZO ULIOISHA KWA MATOKEO YA
MBILI KWA MBILI .
WAFUNGAJI WA REAL WALIKUWA ISCO PAMOJA NA PEPE HUKU OSASUNA
WAKIFUNGA KUPITIA KWA ORIOL RIERA.
KWINGINEKO FC BARCELONA WALIWAFUNGA VILLAREAL MABAO MAWILI KWA
MOJA .
MABAO YA BARCA YALIFUNGWA NA NEYMAR AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI
HUKU VILLAREAL WAKIFUNGA KUPITIA KWA MATTEO MUSACHIO.
NAO ATLETICO MADRID KATIKA MCHEZO ULIOPIGWA JUMAPILI WALIWAFUNGA
VALENCIA MABAO MATATU BILA .
ATLETICO WALIPATA MABAO YAO KUPITIA KWA DIEGO COSTA AMBAYE
ALIFUNGA MABAO MAWILI NA RAUL GARCIA .
NCHINI UFARANSA VINARA WA LIGI KUU YA NCHINI HUMO PARIS ST
GERMAIN WALIENDELEZA MOTO WAO BAADA YA KUWAFUNGA STADE RENEE KWA MABAO MATATU
KWA MOJA . MABAO YA PSG YALIFUNGWA NA ZLATAN IBRAHIMOVICH , EDINSON CAVANNI NA
THIAGO MOTTA HUKU RENEE WAKIFUNGA KUPITIA KWA ROMAIN ALESANDRINI.
AS MONACO AMBAO WALIKUWA UGENINI WAKICHEZA NA GINGAMP WALIPATA
USHINDI WA MABAO MAWILI BILA . WAFUNGAJI KWENYE MCHEZO HUO WALIKUWA ANTHONY
MATIAL NA LAVIN KUZAWA.
NAO LILLE METROPOLE WALIWAFUNGA BASTIA KWA MABAO MAWILI KWA MOJA
. MABAO YOTE MAWILI YA LILLE YALIFUNGWA NA SALOMON KALOU HUKU LUDOVIC GENES
AKIIFUNGIA BASTIA.
NCHINI ITALIA AS NAPOLI WALIWAFUNGA INTER MILAN KWA MABAO MANNE KWA MAWILI .
WAFUNGAJI KWENYE MCHEZO HUO WALIKUWA GONZALO HIGUAIN , JOSE CALLEJON , DRIS
MERTENS NA BLERIM ZEMAILI HUKU INTER WAKIFUNGA KUPITIA KWA YUTO NAGATOMO NA
ESTEBAN CAMBIASSO.
NCHINI UJERUMANI BAYERN
MUNICH WALIENDELEZA REKODI YAO BORA YA KUSHINDA MECHI MFULULIZO BAADA YA
KUWAFUNGA HAMBURG SV MABAO MATATU KWA MOJA . WAFUNGAJI WA BAYERN KWENYE MCHEZO
HUO WALIKUWA MARIO GOTZE , MARIO MANDZUKICH NA SHEDAN SHAKIRI HUKU HAMBURG
WAKIFUNGA KUPITIA KWA PIERE MICHEL LASSOGA
No comments:
Post a Comment