KTNVerified
@KTNKenya
#KandaBongoMan
works as petrol attendant in Mumias -KENYA
Kanda akiwa na ma fun wake.
KENYA:
Mwana muziki mwenye asili ya Congo Kanda
Bongo Manamewashangaza wakaazi wa eneo la Mumias upande wa Magharibi mwa nchi ya Kenya pale ambapo alipowasili bila kutarajiwa
na kuanza kuhudumia umma wa eneo hilo katika harakati za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Kenya . wakaai wa Mumias walibebwa na tukio la mkali huyo wa miondoko
ya kwasa kwasa pale ambapo alikwenda kwenye kituo cha mafuta cha Magharibi Service Station na kuanza
kuhudumia wateja waliokua wakihitaji mafuta.
Kwa taarifa za mashuhuda wa eneo hilo wanasema Kanda
alifit kiulani mno wakati akihudumia wateja ambao pia walishangaa baadaye
walipogundua wamewekewa mafuta na mkali huyo na hasa wakati wa kulipia
walichowekewa kwenye magari na piki piki,na Kanda hakupoteza muda aliwapa
ujumbe kwamba yuko maeneo hayo kwa show kadhaa maeneo ya Bungoma, Kisumu na
maeneo mengine na nimeamua kuutumia muda wangu wa ziada kua pamoja na wana
jamii ambao ni washabiki wangu nia ni kuataka kusikia kutoka kwao stori za
mafanikio yao bila kusahau changamoto zinazowakabili wakati Kenya
inapoadhimisha miaka 50 ya uhuru wake.
Badaye Kanda akaamua kuingia katika nyumba
kadhaa za eneo la Kakamega na kupanda
miti kama kumbu kumbu yake na kuomba miti hiyo iitwe “Kanda Bongo Man Trees”.
Kanda Bongoman hayuko peke yake ameandamana na baadhi
ya wanamuziki wa bendi yake .
Kanda akiwa na ma fun wake.
No comments:
Post a Comment