Rodrigo
Palacio
LIGI KUU YA ENGLAND ILIENDELEA MWISHONI MWA WIKI HII IKISHUHUDIA
MICHEZO SITA ILIYOPIGWA KWENYE VIWANJA TOFAUTI .
HUKO CRAVEN COTTAGE MANCHESTER CITY WAKIWA KWENYE KIWANGO CHAO
BORA WALIWAFUNGA FULHAM KWA MABAO MANNE KWA MAWILI .
MANCHESTER CITY WALIFUNGA KUPITIA KWA YAYA TOURE , MARTIN
DEMICHELIS, JESUS NAVAS NA JAMES MILNER HUKU VINCENT KOMPANY NA KIERAN
RICHARDSON WAKIFUNGA MABAO YA FULHAM.
LIVERPOOL WAKIONGOZWA NA MSHAMBULIAJI WAO TEGEMEO LUIS SUAREZ
WALIWAFUNGA CARDIFF CITY MABAO MATATU KWA MOJA .
SUAREZ ALIIFUNGIA LIVERPOOL MABAO MAWILI NA KUFIKISHA IDADI YA
MABAO KUMI NA TISA HUKU RAHEEM STERLING AKIFUNGA KWENYE MECHI YA PILI
MFULULIZO.
MANCHESTER UNITED WAKIWA KWENYE UWANJA WA OLD TRAFFORD
WALIWAFUNGA WEST HAM UNITED MABAO MATATU KWA MOJA . WAFUNGAJI WA UNITED
WALIKUWA DANNY WELBECK , ADNAN YANUZEI NA ASHLEY YOUNG HUKU WEST HAM UNITED
WAKIPATA BAO LAO PEKEE KUPITIA KWA MSHAMBULIAJI CARLTON COLE.
NCHINI HISPANIA ATLETICO MADRID WALIENDELEA KUWANG’ANGANIA
VINARA WA LIGI HIYO FC BARCELONA BAADA YA KUVUNA POINTI TATU MUHIMU
ZILIZOTOKANA NA MCHEZO WAO DHIDI YA LEVANTE AMBAPO ATLETICO WALISHINDA KWA
MABAO MATATU KWA MAWILI .
DIEGO COSTA WA ATLETICO ALIIFUNGIA TIMU YAKE MABAO MAWILI HUKU
WAJINA WAKE DIEGO GODIN AKIONGEZA BAO LINGINE
NA LEVANTE WALIFUNGA KUPITIA ANDREA IVANISH NA PEDRO RIOS.
FC BARCELONA KATIKA MCHEZO ULIOPIGWA HAPO JANA WALIWAFUNGA
GETAFE MABAO MATANO KWA MAWILI .
GETAFE NDIO WALIOANZA KUFUNGA KUPITIA KWA LISANDRO LOPEZ NA
SERGIO ESCUDERO NA PEDRO RODRIGUEZ ALIIFUNGIA BARCA MABAO MATATU HUKU CESC
FABRIGAS AKIFUNGA MABAO MAWILI .
REAL MADRID WALISAFIRI HADI HUKO ESTADIO MESTALLA AMBAKO
WALIKUWA WAGENI WA VALENCIA .
MCHEZO HUO ULIISHA KWA USHINDI WA MABAO MATATU KWA MAWILI KWA
REAL MADRID .MABAO YA REAL YALIFUNGWA NA ANGEL DI MARIA , CRISTIANO RONALDO
NA JESSE RODRIGUEZ HUKU PABLO PIATTI NA JEREMY MATHIU WAKIFUNGA MABAO YA
VALENCIA .
NCHINI ITALIA JUVENTUS MAARUFU KAMA KIBIBI KIZEE CHA TORINO AKA
THE OLD LADY WALIPATA USHINDI WAO WA TISA MFULULIZO BAADA YA KUWAFUNGA ATALANTA
BERGAMO KWA MABAO MANNE KWA MOJA .
WAFUNGAJI WA JUVENTUS KATIKA MCHEZO HUO ULIOPIGWA JANA WALIKUWA
ARTURO VIDAL , CARLOS TEVEZ , FERNANDO YORENTE NA ANDREA BARZAGLI HUKU MAXIMILIANO
MORALEZ AKIIFUNGIA BAO PEKEE ATALANTA.
NAO AS ROMA WALIENDELEZA WIMBI LA USHINDI SAFARI HII WAKIWAFUNGA
CATANIA MABAO MANNE BILA .
WAFUNGAJI WA ROMA WALIKUWA BEKI WA KIMATAIFA WA UFARANSA MEHDI
BENATIA AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI , MATIA DESTRO NA GERVINHO .
KWINGINEKO FIO
RENTINA WALIWAFUNGA SASSUOLO KWA BAO MOJA BILA .
BAO HILO PEKEE LILIFUNGWA NA MSHAMBULIAJI ANAYEONGOZA KWA
UFUNGAJI KWENYE LIGI YA ITALIA KWA SASA GIUSEPPE ROSSI.
NAO INTER MILAN WALIWAFUNGA AC MILAN KWA BAO MOJA BILA .
BAO HILO LILIFUNGWA KWA MTINDO WA AINA YAKE NA MSHAMBULIAJI WA
KIMATAIFA WA ARGENTINA RODRIGO PALACIO.
NCHINI UFARANSA MABINGWA WATETEZI PARIS ST GERMAIN NA LILLE METROPOLE WALITOKA SARE YA MABAO
MAWILI KWA MAWILI .
MABAO YA PSG YALIFUNGWA NA ZLATAN IBRAHIMOVIC NA MARKO BARSA ALIYEJIFUNGA MWENYEWE HUKU
LILLE WAKIFUNGA KUPITIA KWASALOMON KALOU NA RIO MAVUBA .AS MONACO WALIZIDI KUWEKA SHAKANI MATUMAINI YAO YA KUTWAA
UBINGWA BAADA YA KUKUBALI KIPIGO CHA MABAO MAWILI KWA MOJA MBELE YA VALENCIENNE
.
MABAO YA VALENCIENE YALIFUNGWA NA DAVID DUCUTOX NA ERIC ABIDAL
AMBAYE ALIJIFUNGA MWENYEWE HUKUJAMES RODRIGUEZ AKIFUNGA BAO PEKEE LA MONACO.
No comments:
Post a Comment