Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akipokea Rasimu ya pili ya Katiba Mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya
Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo
iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete
aliitaka Tume hiyo ya Katiba kuhakikisha kuwa Rasimu hiyo inawekwa kwenye
mitandao yote ya kijamii ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa na kuweza
kutoa maoni yao kwa urahisi kupitia mitandaoni.
Rais wa Zanzibar Dkt.
Ali Mohamed Shein akipokea Rasimu ya pili ya Katiba Mpya kutoka kwa Mwenyekiti
wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kukabidhiwa
rasimu hiyo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi kwa Rais,Rasimu ya Pili
ya Katiba iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya
Katiba,Jaji Joseph Sinde Warioba akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya
kukabidhi kwa Rais,Rasimu ya Pili ya Katiba iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya
Karimjee,jijini Dar es Salaam.Jaji Warioba alisema kuwa kulingana na idadi ya
kura zilizopatikana kutoka kwa wananchi kuhusu uundwaji wa Serikali tatu,
alisema kuwa idadi kubwa zaidi ni ya watu waliohitaji Serikali tatu kuliko
walioipinga, hivyo Serikali tatu haipingiki ambapo kwa sasa itabaki ni kazi ya
maamuzi ya Bunge la Katiba linalotarajia kuundwa mapema mwezi Januari mwakani.
Bofya hapo chini ili
kuishusha Rasimu ya katiba mpya
RASIMU ya katiba mpya
Chanzo: Issamichuzi
Blog
No comments:
Post a Comment