Swagg is on
UPO?
Habari Mdau!
MUONGOZAJI bora wa filamu Swahiliwood Jackson Kabirigi ‘Jack’
anawashukru wadau wote wa tasnia ya filamu kwa ujumla wake kutokana na mchango
wake ambao wamempa kupitia kazi zake ambazo ameshiriki katika kuigiza na
kuongoza sambamba na filamu ya Mdundiko iliyomletea sifa baada kuchaguliwa
nchini Marekani.
Akiongea na wanahabari msanii huyo ambaye ana sifa za kimataifa
amesema kuwa baada ya filamu yake ya Mdundiko kushinda tuzo nje ya nchi na si
ndani ya nchi ambapo hata tuzo za ZIFF ilinyimwa, lakini Jack anasema kuwa
amejifunza mengi na anatoa shukrani kwa wadau wa filamu ambao wamekuwa bega kwa
bega katika kuhakikisha anasonga mbele kisanaa.
“Nawashukru wote wanahabari jamaa zangu hata wale ambao wamekuwa
wakinishauri kupitia njia mbalimbali, kila mtu kwangu ana mchango mkubwa sana
naheshimu hilo kwa kila mtu kwa nafasi aliyo nayo na kuhakikisha wanafanya
jambo kubwa kwa ajili yangu mimi Jack nasema Asanteni sana na Mungu
awabariki,”anasema Jack.
Aidha msanii huyo ameamua kuanzisha utaratibu wa kutoa taarifa
za maendeleo ya kazi yoyote ambayo atakuwa akiifanya na taarifa kuwafikia
wapenzi wa filamu nchini nzima na kuwa ndio njia ya wasanii kujenga mahusiano
mema na watazamaji wao ambao kuna wanataka kujua maisha ya wasanii ya kawaida
nje ya uigizaji lakini si rahisi.
Jack pia anawashukru sana wapenzi wa filamu Swahiliwood baada ya
kuipokea kazi yake vema ya Kisate filamu iliyoingia sokoni hivi karibuni na
kufanya vizuri kwa kuteka soko la filamu Bongo, sinema hiyo kaongoza na kuigiza
mwenyewe akishirikiana na wasanii wengine wakali kama Tino, Dino, Dennis, Mzee
Magari, Hamis Korongo na wasanii wengine wanofanya vizuri.
Msanii huyo ana filamu nyingi sana lakini yeye amechagua filamu
kadhaa kuwatambulisha wanahabari na wadau wote kwa ujumla, sinema hizo ni
My Nephew, Money Transfer, filamu hizo kaigizia Afrika ya kusini, Born to
Suffer, filamu ya Nunda, The Close, Home village,Ania.
Filamu zingine ambazo kaingiza na kuzingoza ni Filamu ya
Hatia Nguvu ya Imani, CID, Single O, Kigodoro, Kisate na filamu bora ya
Mdundiko hizi ni baadhi ya filamu ambazo zote zipo katika ubora wa juu na
ameahaidi kufanya mambo makubwa mwaka ujao.
Kazi nzuri ya Jack kutoka Bongo filamu yake aliyoongoza ya
Mdundiko kuibuka kama filamu bora iliyofanikiwa katika kipengere cha mafanikio
ya hadithi katika filamu (Achievement Narrative in Feature Film) ni ushindi
mkubwa kwa mapinduzi ya filamu Bongo Movie. Huyu ndio Jackson Kabirigi
muongozaji wa filamu wa Kimataifa
“NAWAPENDA SANA NAOMBA USHIRIKIANO HUU UENDELEE MIMI NI KIJANA
WENU SITOWAANGUSHA KATIKA KULETA MAPINDUZI YA KWELI YA FILAMU TANZANIA MUNGU
AWABARIKI NYOTE,” Jackson Kabirigi. 05.December. 2013
No comments:
Post a Comment