WANAFUNZI
16,482 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu wamekosa nafasi za
kujiungana kidato
cha kwanza, kutokana na uhaba wa shule za sekondari nchini. Idadi hiyo ni kati
ya wanafunzi
427,609 waliofaulu mtihani huo uliofanyika Septemba 11, katika maeneo
mbalimbali
nchini,
ambapo wanafunzi 411,127 wamechaguliwa kujiunga na sekondari.
Matokeo
hayo yalitangazwa jijini Dar es Salaam
na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini, wakati akizungumza na waandishi
wa habari.wannafunzi
Sagini alisema wanafunzi waliokosa nafasi wanatoka katika
mikoa
minane, ikiongozwa na Dar-es -Salaam yenye wanafunzi 11,796, Mbeya 1,484,
Geita1,578,
Dodoma 549, Njombe 379, Morogoro 315, Katavi 261 na Mtwara120.
Alisema
wanafunzi waliokosanafasi watasubiri hadi Februari mwakani, iwapo watapata
shule
katika
uchaguzi wa awamu ya pili kutokana na baadhi ya wanafunzi kwenda katika shule
binafsi.
“Haiwezi
kuwa ni furaha kusema wengine wamepata na wengine wamekosa, tayari tumeziagiza
halmashauri
zilizobakiza wanafunzi kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwawezesha
wanafunzi hao kujiunga kidato cha kwanza ifikapo Machi, mwakani.
“Hii si
ya mara ya kwanza kwa wanafunzi wa darasa la saba wanaofaulu kukosa nafasi za
sekondari,
kwani mwaka jana baadhi ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo katika mikoa ya
Arusha,
Njombe na Mwanza walikosa nafasi. “Katika Mkoa wa Arusha wanafunzi 6,838
walikosa nafasi, wakati Njombe ni wanafunzi 800 na Mwanza 1,400,” alisema. Sagini
aliwahimiza wazazi, walezi na
viongozi wa wilaya husika kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa
wanaandikishwa
na
kubakia shuleni hadi watakapohitimu elimu ya sekondari.
Katika hatua nyingine, Saginialisema kuanzia
sasa, mtoto yeyote atakayefika darasa la tatu kama atakuwa hana sifa za kuingiadarasa
la nne, atalazimika kurudia darasa.Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa idadi kubwa
ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma, kuandikana
kuhesabu. Kulingana na matokeo ya utafiti yaliyotangazwa hivi karibuni na taasisi
isiyo ya kiserikali ya Uwezo Tanzania (TWAWEZA), inaonyesha kuwa asilimia 24 ya
wanafunzi wa darasa la saba hawawezi kusoma hadithi rahisi ya wanafunzi wa darasa
la pili iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Utafiti
huo pia ulibaini kuwa asilimia 50 ya wanafunzi hao hawawezi kusoma hadithi ya Kiingereza
ya darasa la pili na asilimia 11 hawawezi kufanya hesabu rahisi za darasa la
pili. Taarifa nyingine iliyotolewa juzi na Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi
(TAMONGSCO), ilieleza kuwa zaidi ya
wanafunzi
12,000 waliofanya mtihani wa darasa la saba hawajui kusoma.
No comments:
Post a Comment