UTANGULIZI
JITAMBUE NA UJIAMINI NI PROJECT
INAYOFANYWA NA MTANGAZI WA REDIO YA CLOUDS FM PERFECT CRISPIN CHINI YA KIPINDI
CHA CLUB 10 CHENYE MAUDHUI YA WANAFUNZI KIKIJENHGWA NA NGUZO YA ELIMU NA
BURUDANI YANI EDUTAINMENT LENGO LA PROGRAM HII AMBAYO ITAKUWA INAFANYIKA MARA
KWA MARA KWA UPISHANO WA MUDA MAALUMU NI KUWAJENGEA VIJANA WADOGO UWEZO WA
KUJITAMBUA MAPEMA WAKIWA SHULENI NA UWEZO WA KUJIAMINI POPOTE PALE WALIPO ILI
WAWEZE KUFANIKIWA MAISHANI MWAO KUPITIA ELIMU WATAKAYOIPATA VIPAJI NA VITU
WANAVYOVIPENDA.
LENGO
“JITAMBUE
JIAMINI U CAN DO IT” NI KAULI MBIU INAYOMUAMSHA KIJANA KUJITAMBUA KUJIAMINI NA
KUCHUKUA HATUA KUSONGA MBELE NA LENGO LAKE KUU NI KUJENGA KUNDI LA VIJANA
WANAOJITAMBUA NA KUJIAMINI NCHINI TANZANIA
WAHUSIKA
PROGRAM HII ITAHUSISHA WATOA MADA MBALI
MBALI WAKIWEMO WATU MAARUFU MAKAMPUNI NA WASOMI MBALIMBALI NA WALENGWA WENYEWE
AMBAO NI WANAFUNZI, LENGO KUU LIKIWA LILE MLILE KUWAJENGEA VIJANA WADOGO UWEZO
WA KUFIKIRI (KUJITAMBUA KUJIAMINI NA KUSONGA MBELE)
FAIDA
MWANAFUNZI ATAJIFUNZA VITU MBALI
MBALIKUTOKA KWENYE HII SEMINA KAMA KUFUATA NYAYO ZA WALIOMTANGULIA BAADA YA
YEYE MWENYEWE KUAMUA ANATAKA KUFANYA NINI KATIKA MAISHA YAKE LICHA YA
KUJITAMBUA PIA KUJIPA THAMANI KAMA KIJANA KUPITIA NGUVU ILIYOPO NDANI YA
KUJIAMINI NA PIA UWEZO MKUBWA WA KUJIELEZA POPOTE PALE ANAPOKUWA!
TAFITI
KWA TAFITI NDOGO ILIYOFANYWA NA KIPINDI
CHA CLUB10 INAONYESHA WATU WAZIMA ASILIMI KUBWA WANASHINDWA KABISA KUJIELEZA
KWENYE JAMBO LOLOTE AMBALO WANATAKIWA KUJIELEZA
VIVYO SAMBAMBA NA ASILIMIA KUBWA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU ELIMU YA JUU
HAWAJITAMBUA NA HAWAJIAMINI!
HITIMISHO
BAADA YA KUFANYA TAFITI NYINGINE NDOGO
KUJUA TATIZO LINAANZIA WAPI TUMEKUJA KUJUA TATIZO LINAANZIA SHULE ZA AWALI
WATOTO WAKIWA WADOGO HAKUNA MITAHALA AU UTARATIBU WA KUJENGEA WATOTO UWEZO WA
KUJIAMINI NA KUJITAMBUA KATIKA HATUA ZA AWALI JAMBO LINALOKUJA KUWA TATIZO
UKUBWANI MWAO KWA KULIONA HILO CLUB 10 YA CLOUDS FM CHINI YA PERFECT CRISPIN NA
WADAU WENGINE WAMEAMUA KUANZISHA PROGRAM HII MUHIMU YA JITAMBUE JIAMINI U CAN
DO IT KWA MATUNDA MEMA YA NCHI YA
BAADAE!!
No comments:
Post a Comment