TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete , Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteuaKamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi BaloziOmbeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi yaMkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake
unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014,Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa
Inteligensia ya Jinai(Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la
Polisi.Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteuaKamishna
Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi,ambayo ni nafasi mpya
katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake,
Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna waUchunguzi wa Kijinai (Commissioner for
Forensic Investigations).Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho,
Jumanne,Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
30 Desemba, 2013
No comments:
Post a Comment