Mifuniko ya tenki la
mafuta ikiwa imefunguliwa baada ya kutolewa vipodozi
Ndani ya lori hilo
baada ya kutolewa vipodozi hivyo
Kamanda wa polisi mkoa
wa Iringa Ramadhan Mungi akionyesha shehena ya
vipodozi ambavyo
vimekamatwa vikisafirishwa ndani ya lori la mafuta leo.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Iringa ,Ramadhan Mungi akionyesha lori la mafuta lililokuwa na shehena ya
vipodozi.
Jina la kampuni
linalomiliki lori hilo
Maofisa wa mamlaka ya
chakula na dawa Manispaa ya Iringa wakikagua vipodozi hivyo.
JESHI la polisi mkoa wa
Iringa limewakamata watu wawili akiwemo dereva wa tenki la mafuta lenye namba
za usajili T 247 BHP wakisafirisha shehena ya vipodozi maboksi 779 vikiwa
vimewekwa ndani ya tenki hilo la mafuta kutoka nchi za kusini mwa Tanzania
kuelekea jijini Dar es Salaam .(P.T)
Kamanda wa polisi wa
mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa lori hilo lenye namba za usajili T
247 BHP likiwa na tela lenye namba T 598 BMK ni mali ya kampuni ya World OIL
Ltd ya Jijini Dar es Salaam lilikuwa likiendeshwa na Mohamed Sadru (23) mkazi
wa Mbezi Temboni jijini Dar es Salaam .
Mbali ya dereva huyo pia
jeshi hilo linamshikilia mfanyabiashara aliyekuwa akisafirisha mzigo huo Bw
Kassim Kaifa (23) mkazi wa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika na mzigo
huo.
Kamanda Mungi
aliwaeleza wanahabari leo kuwa mtego wa jeshi la polisi uliweka baada ya kupokea
taarifa kutoka kwa rai wema kuhusiana na lori hilo kutumika isivyo kwa
kusafirisha vipodozi hivyo.
Alisema kuwa taarifa
kuhusiana na lori hilo kusafirisha vipodozi badala ya mafuta waliitapata kutoka
jana na mtego wa kulikamata lori hilo umefanikiwa majira ya saa 9 alfajiri ya
leo
Hata hivyo alisema kuwa
sehemu kubwa ya vipodozi hizo ni vile ambavyo vilipigwa marufuku na serikali
kutokana na kuwa na madhara makubwa kwa afya ya watumiaji wa vipodozi hivyo.
Alisema kuwa jeshi la
polisi limefanikiwa kumata vipodozi hivyo kwa kushirikiana na mamlaka ya
chakula na dawa ,wakala wa barabara mkoa wa Iringa na mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA)
Kamanda huyo alisema
kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika
na kuwa ni mapema kwa sasa kuitaja thamani ya vipodozi hivyo na nchi ambayo
lori hilo lilikuwa likitoka kutokana na sababu za kiusalama.
KWA HISANI KUBWA YA HABARI KWANZA! ASANTE SANA
No comments:
Post a Comment