Wednesday, December 18, 2013

AJALI KAZINI





Dunia kweli ina majanga, na ajali kazini ni jambo linaloelekea kua la kawaida sasa! Ila mbele wametisha, kwani badala ya kukitupa kiungo kilichokatwa na mashine isivyo bahati, sasa wanakipachika sejemu ili kisife na hivyo baadae watakirejesha sehemu husika.

Mwanamume mmoja ambaye mkono sehemu ya juu ya kiganja imefyekwa na mashine alipokua katika utendaji wake wa kawaida,kwa sasa umeegeshwa kwa muda wa mwezi mmoja kabla hajafanyiwa upasuaji na kukirejesha.
Madaktari walimwambia bwana Xiao Wei kwamba wana tatizika kumsaidia kwa namna alivyofyekwa siku ya tarehe 10 November mwaka huu.

Xiao alipata ajali hiyo katika jimbo la  Hunan , huko China, Mr Xiao akaeleza alivyojisikia baada ya ajali hiyo! anasema “I was just shocked and frozen at the spot, until co-workers unplugged the machine and retrieved my hand and took me to the hospital.upo kauli yake hiyo bila ya kuichakachua

Katika mazingira ya kawaida mno ukiwa kijana halafu upoteze kiungo cha mwili wako unajiona una kasoro kubwa, ni afadhali ungezaliwa hivyo ungezoea

Mnamo tarehe  10 December madaktari wakakubaliana kwamba bwana Xiao anaendelea vyema na hivyo uwezekana wa kuurejesha mkono huo upo ingawa atakabiliwa na oparesheni kadhaa ili kuufanya uwe katika hali bora zaidi.

Ndivyo ulivyoungwa


No comments:

Post a Comment