Mwanamume mmmoja
aliamua kuchukua maamuzi yasiyotegemewa na wengi kutokana na tabia ya mpenzi
wake kupenda manunuzi kupitiliza,na hasa mavazi!
Ama kwa hakika
ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni!camera za
CCTV zilionesha namna Tao Hsiao,aliyekua na umri wa miaka 38, alivyokua akimsindikiza mpenzi wake duka
hadi duka kwa manunuzi katika shopping mall iliyoko katika mji wa Xuzhou,katika jimbo la Jiangsu ,Mashariki mwa nchi ya China.
Katika sindikiza hiyo
ilochukua saa tano,mpenzi wa Tao,bado alikua na mzuka wa chukua hiki acha kile,
Tao akachoka na kudai waanze safari ya kurejea nyumbani.
Shuhuda kila pahala
penye tukio huwa hakosekani,shuhuda wa tukio hili anadai kua alimsikia Tao
akimwambia mpenzi wake kua yatosha na wamesha nunua vitu tele mpaka vinakaribia
kuwashinda kuvibeba,lakini mpenziwe akazidi kung’ang’ana kuingia duka la mwisho
kabla ya kuondoka kwasababu kulikua na punguzo la bei kwenye bidhaa ya viatu
ambavyo vinadumu
Mjengo ambao Tao alijiachia!
Tao alipolalama kwamba
yatosha,mpenziwe aliamua kufungua mdomo wake na kumfokea kwa sauti kubwa mno! Huku
akimtuhumu kutaka kumharibia sikukuu kubwa ijayo ya Christmas,kauli iliyo
muumiza mno Tao.
Katika msongo huo, Tao akaamua kubwaga sakafuni
bidhaa zote walizonunua awali na kasha kuamua kwenda kwenye balcony, akakumba
mapambo ya Christmas yalokua yako huko na kasha kujitupa kutoka orofa ya saba
na kuwaacha walio wengi wakiwa hawaamini macho yao.
Kitengo cha uokozi
kilipotinga eneo la tukio, kilikuta Tao akiwa amekwisha aga dunia kwa kitendo
chake cha kujitupa na hivyo basi mwili wake ukachukuliwa fasta kwenda
kuhifadhiwa.
No comments:
Post a Comment