Monday, December 30, 2013

MAKAMBA AWASIHI BODABODA WA MWANZA: URAHISI NA UHARAKA WA UPATIKANAJI LESENI USIWE TIKETI YA VIFO VYA WANANCHI.

NAIBU wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba ametaka ujio wake Jiji la Mwanza usihusishwe na Kampeni za chini kwa chini za Urais bali ni kutekeleza ombi la Umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza kuwasaidia kupata Bima ya Afya baada ya kuwawezesha kupata pikipiki 1745 za FEKON na si vinginevyo.

Kauli hiyo ya Makamba ameitoa leo wakati wa kufungua kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini hapa, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji ujio wangu Mwanza “Niko hapa kwa ajili ya shughuli hii mliyonialika bali kuja kushiriki Kampeni muhimu ya Bima ya Afya kwa ajili ya Usalama wa badae” na si vinginevyo.

Makamba amesema kwamba upatikanaji wa Leseni kwa urahisi na uharaka usiwe tiketi ya Kifo  kwa wananchi (ZAIDI MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)


Awali kabla ya kongamano hilo madereva hao wa bodaboda walifanya maandamano toka makao makuu ya ofisi zao yaliyopo mtaa wa malango mmoja wilayani Nyamagana jijini Mwanza hadi katika uwanja wa historia wa Nyamagana.
Wadau wa Bodaboda wakiingia uwanja wa Nyamagana.
Ndani ya uwanja wa Nyamagana madereva wa Bodaboda wamejitokeza kiasi cha kutosha.
Huku wengine wakizidi kumiminika viwanjani hapa kuhudhuria kongamano lao.
Naibu wa Sayansi na Teknolijia ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mhe. January Makamba akiingia katika uwanja wa Nyamagana kushiriki kongamano la Bima ya Afya kwa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa mkoa wa Mwanza.
Kila mmoja viwanjani hapa alikuwa na kiu ya kusalimiana ana kwa ana na Naibu waziri huyo.
Licha ya kutoa elimu ya uelimishaji kujitambua kwa Bodaboda wa jiji la Mwanza ili kuepukana na maisha magumu uzeeni kwa wadau hao wa usafiri, Mkuu wa mkoa waMwanza Evarist Ndikilo ndiye aliye mkaribisha Mhe. Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia kuhutubia maelfu ya wadau hao. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evaris Ndikilo kabla ya kumkalibisha mgeni rasmi aliwaasa bodaboda kufuata sheria na kanuni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shughuli zao zinafanyika kwa umakini na kwa amani na utulivu huku wakihakikisha usalama kwanza katika kazi zao kwa kuwa wanatumia vyombo vya moto.

Injinia Ndikilo aliwataka pia kufuata sheria za barabarani kutokana na kuwepo watumiaji wengine, kuwa waangalifu na abiria wengine wanaowachukua kutokana na baadhi yao kuwateka na kuwafanyia ukatili, kuwauwa na kuwanyanganya pikipiki zao nyakati za usiku na kuwataka kukataa kushiriki katika shughuli za uhalifu na badala yake wawabaini na kuwatolea taarifa kwa viongozi na jeshi la polisi.

Makamba alisema kuwa kupatikana kwa Bima za Afya kutatawezesha wanaopata ajali kupatiwa matibabu na kupata fidia pindi wanapopata ajali na kupata ulemavu na kifo jambo ambalo ni hakika lazima wakubali kukata bima kutoka Kampuni ya Ndege Insurance na Shirika la Bima la Taifa (NIC) yaliyokubali kuingia mkataba na wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza. 
Ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuachana na tabia ya manyanyaso kwa waendesha pikipiki ya kuwabambikia kesi na makosa bali washirikiane nao kuwabaini walio wachache wanaojipenyeza kujifanya ni bodaboda kumbe ni wanaofanya vitendo vya kihuni, uhalifu na wizi kwa kivuli cha bodaboda jambo ambalo litasaidia pia kuwabaini wanaovunja sheria taritibu zilizopo.
“Mimi leo nimekubali kuwa Mlezi wenu lakini kila kijana lazima amiliki pikipiki yake mwenyewe badala ya kuwa mtu wa kuajiliwa tunahitaji kila mmoja ajiajili kwa kuwa na chombo chake, kazi ya pikipiki iwe ya usalama isiwe leseni ya kifo na ulemavu, msije mkadanganywa na baadhi ya watu kuwa watawatetea bali sisi wa viongozi wa Serikali Taifa, Mkoa, Wilaya na Jiji na kuweni makini kwa kufuata sheria za usalama” alisisitiza
Tangu kuingia mkataba na Kampuni ya Tanzania China Dev Ltd wamefanikiwa kuwakopesha 1745 na awamu ya kwanza umoja umlikopesha pikipiki 265, awamu ya pili 450 na awamu ya tatu pikipiki 1000 na wanachama wapatao 1745 wamenufaika na kupata ajira .
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alikuwa ni mmoja kati ya viongozi walioshiriki zoezi la kuendesha bahati nasibu ya waendesha bodaboda 100 waliobahatika kuandikishwa Bima ya Afya bure katika kongamano hilo.
Zoezi la bahati nasibu ya Bima ya Afya linaendelea na waliobahatika ndiyo hawa waliokuwa wakifika mbele katika mstari.
Mwakilishi toka jeshi la polisi na bahati nasibu ya Bima ya Afya.
Kongamano hilo limelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya kufuata sheria za usalama barabarani, kusoma na kupata cheti na hatimaye leseni, kuhimiza kuvaa kofia ngumu, kuhimiza kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuhimiza waendesha pikipiki kufuata taratibu zote zilizowekwa na serikali kwa wanachama wa wilaya za Sengerema, Nyamagana, Ilemela , Kwimba, Ukerewe, Magu na Misungwi.
Ndikilo kusanyikoni.

Burudani ndani ya Kongamano hazikukosekana.
Wadau walikuja na vyombo vyao.
No Parking.

No comments:

Post a Comment