Friday, December 20, 2013

FIFA YAMRUHUSU OKWI KUJIUNGA NA YANGA







Mkurugenzi wa mashindano wa
chama cha soka cha Uganda
Decolas Kiiza, amethibitisha
kwamba shirikisho la soka duniani
FIFA limeridhia usajili wa
mshambuliaji Emmanuel Okwi
kujiunga na klabu ya Yanga.
“Ndio tuliandika barua FIFA na
wametujibu kwamba mchezaji
yupo huru kwa kusajiliwa na timu
yoyote,"Kiiza alisema.
Mapema wiki hii CEO wa FUFA,
Edgar Watson, alisema kwamba
waliwasiliana na FIFA ili kupata
maelezo juu ya uhalali wa usajili
wa Okwi.
Yanga walikamilisha usajili wa
Okwi mapema wiki hii kwa
mkataba wa miaka miwili na huku
ikiwa bado aliruhusiwa na FIFA
kujiunga na SC Villa kwa muda
maalum akitokea Etoile du Sahel.
Okwi tayari amewasili nchini
akitokea Uganda kuja kujiunga na
klabu ya Yanga mapema leo
mchana.
Allan Papaok, mkurugenzi wa
kampuni ambayo inashughulikia
haki za Okwi, alisema leo kwamba
bado hawajakamilisha usajili wa
Okwi na YANGA.
“Tutasafiri kwenda Dar es salaam
wikiendi hii kwa ajili ya
kukamilisha usajili huu," aliongeza
bwana Allan Papaok.
Hata hivyo maofisa wengi wa
chama cha soka cha Uganda
wanashangaa ni namna gani FIFA
inaweza kumruhusu Okwi kujiunga
na Yanga, wakati akiwa
ameruhusiwa kujiunga na SC Villa
kwa muda maalum kutoka Etoile
du Sahel, ambao walikuwa na
matatizo na Okwi.

No comments:

Post a Comment