DAR -ES -SAALAM.
Rais Jakaya Kikwete
ametia saini hati ya dharura (Certificate of Urgency) ili Muswada wa Fedha wa
Mwaka 2013 ufanyiwe marekebisho ya kuondoa tozo ya kodi kwa kadi za simu.
Bunge la Bajeti kwa
mwaka wa fedha wa 2012/13 lilipitisha kodi ya Sh1,000 kwa kila kadi ya simu,
hatua ambayo ilipingwa na wabunge wengi.
Ingawa wasemaji wa
Ikulu hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa Rais Kikwete alitia
saini hati hiyo juma hili.
Ingawa wasemaji wa
Ikulu hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa Rais Kikwete ametia
saini hati hiyo juma hili.
“Maana yake ni kuwa,
muswada huo unatakiwa urudi bungeni haraka ili uweze kufanyiwa marekebisho
hayo,” alisema Makamba. Alisema kabla ya kufikiwa kwa hatua hiyo, Rais
alishawaagiza wadau wanaohusika na sekta hiyo wakae na kujadili suala la kodi
hizo... “Mazungumzo hayo bado yalikuwa yanaendelea mpaka katikati ya juma
hili.”
Hata hivyo, alisema
suala la muswada huo kurudishwa bungeni linategemea na ratiba huku akisisitiza
kuwa
licha ya Bunge
kupitisha muswada huo tangu Julai, mwaka huu, bado kodi hizo zilikuwa
hazijaanza kutozwa.
Julai 23, mwaka huu,
Rais Kikwete aliagiza mamlaka zinazohusika na kodi na mawasiliano pamoja na
kampuni za simu za mikononi, kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza
mvutano wa kodi hiyo.
Alitoa kauli hiyo
alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano Sayansi na
Teknolojia na wawakilishi wa kampuni za simu za TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na
Zantel, Ikulu, Dar es Salaam.
Alisema lengo kuu la
kukutana huko lilikuwa ni kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la Sh178 bilioni
ambazo zitapotea katika bajeti iwapo kodi hiyo itafutwa.
Wakati wa mvutano wa
kodi hiyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alinukuliwa na vyombo vya habari akisema
tozo hiyo haikuwa ya kuwaumiza wananchi, bali mapato yake yalilenga kwenda moja
kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Bajeti, Andrew Chenge alinukuliwa akisema uamuzi kuhusu kodi ya kadi za simu
haukuwa wa kubahatisha na kwamba kamati yake ilifanya utafiti wa kina na kisha
kufikia uamuzi wa kuona tozo hiyo ni sahihi.
No comments:
Post a Comment