Na Jeshi la polisi nchini BRAZILI limeendelea na kibarua kizito cha kulitawanya
kundi la waandamanaji waliokua wakielekea katika uwanja uliopo kusini mashariki
mwa jiji la FORTALEZA kwa ajili ya kuzuai mechi hiyo isifanyike kati ya SPAIN
na ITALY.
Waandamanaji hao zaidi ya
5000 walikua wanakaribia kabisa katika
uwanja wa CASTELAO dakika chache kabla ya mchezo wa kombe la shirikisho kuanza hata hivyo baada ya kuzuiwa na jeshi la
polisi walianza kuchoma magari yanayomilikiwa na serikali nchini humo pamoja na
kufanya vurugu huku wakiipinga serikali yao kwa kuwekeza pesa nyingi katika
maandalizi ya kombe la dunia ili hali nchi yao inakabiliwa na ukosefu wa elimu
bora pamoja na afya.
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha televisheni cha SKY NEWS
alikuwepo katika kadhia hiyo.
Pamoja na vurugu hizo kutokea lakini mchezo ulipigwa kati ya SPAIN na ITALY ambapo mpaka dakika ya 90 timu hizo
zilitoshana nguvu na hata baada ya dakika za nyongeza lakini hali ilibadilika
mara baada ya timu hizo kuanza mikwaju
ya penalty na hatimaye ITALY ilijikuta ikitupwa nje baada ya kufungwa na SPAIN
kwa mikwaju ya penalty 7 kwa 6
No comments:
Post a Comment