MAHOJIANO
Karibu
katika sehemu hii ya pili na ya mwisho katika mahojiano kati ya Jamii
Production na Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum
Ali yaliyofanyika Juni 9, 2013.
Katika
sehemu hii, Mhe. Balozi Amina amezungumza mengi ikiwa ni pamoja na....
1:
Nafasi ya wanawake katika maamuzi na maendeleo ya Afrika. Je! Idadi kubwa ya
wanawake tulionao katika nyadhifa barani Afrika ni ishara ya maendeleo ama ni
"nafasi za upendeleo"?
2:
Anaitafsiri vipi DEMOKRASIA YA AFRIKA na anaamini kipimo cha Demokrasia barani
Afrika kingekuwa nini?
3:
Ni nini anachoamini kuwa kingefanyika barani Afrika ili kuleta demokrasia ya
kweli?
4:
Anaamini Umoja wa Afrika umefanikiwa kwa kiasi gani katika madhumuni ya
kuanzishwa kwake?
5:
Je! Anaamini kuwa RUSHWA itaisha barani Afrika?
6:
Yeye kama Mwanasiasa, Mwanadiplomasia na mTanzania, anazionaje siasa za
Tanzania kuelekea 2015?
7:
Anaishauri nini serikali katika kukabilaiana na ukuaji wa TEKNOLOJIA YA HABARI?
8:
Kutokana na hali ilivyo Tanzania hivi sasa, anaionaje nafasi ya mwanamke katika
kuongoza Tanzania?
9:
Nini wito wake kwa wale wote wanaofuatilia mahojiano haya?
KARIBU
UUNGANE NASI
No comments:
Post a Comment