Thursday, June 27, 2013

HII NI KWA TAARIFA YAKO TU


                                                            JANUATY MAKAMBA





January Y. Makamba

Kama ambavyo tayari ilitangazwa awali, siku ya Jumatano, tarehe 10 mwezi Julai mwaka huu namba zote za simu (SIM cards) ambazo hazijasajiliwa zitakuwa si halali kuendelea kutumika na zitasitishwa matumizi yake.

Zoezi la kusajili namba za simu ambalo linaendelea bado halijafanyika kikamilifu kwani zipo namba nyingi zinazotumika ambazo bado hazijasajiliwa na pia uwepo wa watu wengi kutumia majina na vitambulisho bandia kwenye usajili. Baadhi ya mawakala wa usajili wamekuwa wakichangia uwepo wa tatizo hili kwa kutohitaji vitambulisho stahiki toka kwa wanaoomba kusajiliwa.

 Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inashirikiana na Jeshi la Polisi na Mamlaka nyingine za sheria kuwawajibisha wale wote wanaokiuka sheria za usajili na matumizi sahihi ya simu.
HAKIKISHA LINE YAKO YA SIMU (SIMU CARD) IMESAJILIWA KABLA YA SIKU YA JUMATANO TAREHE 10 MWEZI JULAI, 2013.

    Stanslaus Chahe Tumekupata mheshimiwa

    Daniel Waziri Umesomeka kaka @january

    Philemon Kisinini Kuna hawawaliosajili kwa majina ya Freemason Tempu, Freemason Shetani Mheshimiwa hebu tafakari hili suala ni akili kweli kukubali kusajili namba yenye jina kama hili? matokeo yake wanatusumbua mchana na usiku kwa kupigapiga ovyo halafu hawasemi kitu zaidi ya upuuzi tu

    Dennis MpendaMungu Tunashukuru kwa Taarifa mh ila bado Wananchi wako wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye Swala la Usajili hasa wale waliopoteza Vitambulisho vyao na kupelekea Kusajili line zao kwa Vitambulisho vya ndugu Jamaa na Marafiki hivyo, Serikali kwa kushirikiana na TCRA iangalie namna ya kulisaidia kundi la awali lililokosea kwa kutumia Vitambulisho ambavyo c vyao kwani, kundi hili ni kubwa zaidi kuliko lile linalokisiwa kwamba, halijasajili kabisa.

    Ernest Paul Sebarua Mimi tatizo langu ni sms za bure toka kwenye mitandao ya cm. ANGALIENI UWEZEKANO WA KUFUTA SMS za bure kwani zinatumika kuleta uchochezi utakaoligharimu TAIFA LETU. Ni bora mlaumiwe leo kwa kufuta sms za bure kuliko msubiri kulaumiwa kesho kwa kushndwa kuzuia uchochezi huu. Mh hz sms za uchochezi znasambaa kwa haraka kwasababu ni za bure lakini zikiwa ya kulipia watu hawatatuma. Jambo la 2 kuhusu hzi sms za bure ni kuwaweka aBIZE WADOGO ZETU WANAFUNZI MUDA WOTE wanabofya cm wakichat kwa sms kwasababu ni za bure. CHONDECHONDE PIGENI MARUFUKU SMS ZA BURE tena ikiwezekana bei ya sms iongezwe
   
    Simba Deogratias Ni taarifa muhimu. Changamoto ni kwamba hata tuliokwishasajiliwa tunapokea ujumbe kwamba SIM card zetu hazijasajiliwa, ukijaribu kuhakiki kwa kubonyeza ile reli 106 nyota ... unapata jina lako. Inatunganyanyi kwelikweli!

    Fungo Augustus MheJanuary Y. Makamba kwanza nikupongeze jinsi unavyowajibika lakini bado nashindwa kuelewa umuhimu wake ikiwa nimesajili line yangu kwa maana ya kuchukua majukumu yote yanayohusika na line hiyo kwa maana ikitumika vibaya lakini hiyo hiyo mitandao ya simu,nisipoitumia kwa mwezi mmoja wanaifunga afu wanampa mtu mwingine au wakati fulani kwakuwa tu mtu una namba nzuri kuna michezo inafanyika mnajikuta namba moja hiyo hiyo mko watu wawili labda tu PUK inakuwa tofauti kwa nini hili lisithibitiwe ili mtu akisajili line abaki nayo hiyo?
 
    Edward Mgaya Kaka hill zoezi mmekuwa mkiliahirisha kila kukicha mpaka lini? Vyombo vya habari Leo vimesema zoezi litafanyika Julai 31, wewe sasa hivi unasema Julai 10. Which is which?
   
    Elma Frank zoezi hili linaboa, manake namba zangu zote nilizisajili ofisini kwa mashirika ya simu wala sio kwa wakala lakini naambiwa usajili haujakamilika, inaboa sana na niusumbufu mkubwa. Customer care ni mbovu nikifikiria tena kuingia kwenye hizo ofisi napata shida sana.

No comments:

Post a Comment