Rais JAKAYA KIKWETE NA BAN KI MOON
Rais JAKAYA KIKWETE amelaani kwa mara nyingine vitendo “vya aibu” vya mauaji ya albino kwa sababu za kishirikina, akiapa kuwa Serikali itahakikisha kuwa aibu hiyo inakomeshwa kabisa nchini.
Mtoto albino, mmoja wa wanaoathiriwa na mauaji hayo alokemea rais
Amefafanua kuwa tatizo la mauaji ya albino katika Tanzania siyo tatizo la haki za binadamu wala tatizo la ubaguzi, bali ni tatizo la ushirikina ambao umevuka mipaka.
Rais Kikwete amelaani vitendo hivyo vya mauaji ya albino wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon ambaye alitaka kujua maendeleo yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na mauaji ya albino.
Hata hivyo, Rais Kikwete amesisitiza kuwa mauaji ya albino katika Tanzania yamepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka miwili, mitatu iliyopita hata kama hayajaisha kabisa kwa sababu ya hatua kali ambazo zimechukuliwa na Serikali.
Baba na mwana
No comments:
Post a Comment