Friday, June 7, 2013

UNAMKUMBUKA KIBAKULI WA KAOLE SANAA GROUP?


           SADIKIMbelwa a.k.a KIBAKULI




Dar. Mwigizaji wa tamthilia aliyewahi kutamba miaka ya 90 katika kundi la Kaole Sadiki Mbelwa maarufu kama Kibakuli ameibuka upya katika tasnia ya filamu akifanya kazi tofauti kabisa na kipaji chake cha awali.

Akizungumza Kibakuli alisema kwa sasa yeye ni soundman (anayehusika na marekebisho ya sauti katika filamu) kwenye kampuni ya Landline Production na punde anatarajia kurudi tena katika uigizaji.

“Nimekuwa nashika boom na kufanya marekebisho mengine ya sauti katika filamu lakini hivi punde natarajia kurudi tena katika ulimwengu wa filamu watu waendelee kunisubiri tu,” alisema Kibakuli ambaye kwa sasa hana mwili mkubwa kama ilivyokuwa awali.
 SADIKI AKIWA KAZINI

Kibakuli alikuwa staa kwenye maigizo ya Kaole kama mtoto mnoko wa Muhogo Mchungu ambaye anajua kama baba yake ana nyumba nje lakini hamwambii mama yake mzazi.Mwishowe na yeye anakuja kumtaka kimapenzi mama yake mdogo.

Kikubwa kilichokuwa kinamtambulisha Kibakuli ulikuwa ubonge wake, tofauti na sasa amekuwa mwembamba na amekuwa mtu mzima.Kibakuli alianza kuigiza kwenye miaka ya 1999 yupo darasa la sita wakati akiwa na Nyamayao ambaye alikuwa anaigiza kama dada yake.

No comments:

Post a Comment