Tuesday, June 4, 2013

KUHUSIANA NA SUALA LA KATIBA



 

 
Ni rasimu tu lakini... "Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar"
Mapendekezo haya yakivuka hatua ya rasimu yataleta tija kubwa "Tume inapendekeza jina la tume liwe Tume Huru ya Uchaguzi. Tume pia inapendekeza sifa za wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ziwekwe kwenye Katiba. Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi watapatikana kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizoainishwa ndani ya Katiba kwa kuomba"

nimeipenda hii ya mawaziri lazima wawe na elimu ya walau degree moja safi sana tulikuwa tunaongozwa na vilaza.. big up Warioba Mungu ajalie mapendekezo yenu yakubalike mengi yana bamba

JamiiForums wrote:

Kutoka Rasimu ya Katiba Mpya Tanzania:
- Tume inapendekeza mgombea binafsi aruhusiwe!
- Tume inapendekeza Rais asiwe na umri chini ya miaka 40
... - Inapendekezwa Rais aunde Serikali ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi 15 na mawaziri hao wasiwe wabunge!
- Tume inapendekeza mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar




Mambo ya Katiba kama ulimisi mwanawane:

Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania, imependekeza wawepo wagombea huru katika ngazi za uchaguzi mbalimbali nchini.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Warioba amesema pia wapo wananchi waliopendekeza kwamba, wagombea huru waruhusiwe kugombea nafasi zote isipokuwa nafasi ya urais. Jaji Warioba amesema tume ilipitia maoni hayo na kupendekeza kwamba, wagombea huru waruhusiwe kugombea nafasi zote kuanzia ngazi ya Mwenyekiti wa Mtaa hadi nafasi ya Urais.
...
Kadhalika Jaji Warioba amesema, Tume pia imependekeza kwamba, mgombea yeyote wa urais ili athibitike kuwa ni mshindi atalazimika kupata zaidi ya asilimia hamsini ya kura, na kwamba endapo mgombea hatafanikiwa kupata asilimia hamsini uchaguzi utarudiwa kwa kuangalia wagombea wawili waliopata kura nyingi.

Mapendekezo mengine yaliyotangazwa na Tume ni pamoja na kuwepo kwa serikali tatu yaani ya Bara,Zanzibar na ile ya Shirikisho.

Pia tume imependekeza kuwa, Bunge la Muungano liwe na jumla ya Wabunge 75, hamsini kutoka Bara, ishirini kutoka visiwani na watano wateuliwe na Rais kutoka makundi maalum ya walemavu.
Mapendekezo mengine ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni pamoja na Rais kubakia na madaraka yake ya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu, lakini uteuzi wa ngazi za chini uachiwe Tume ya Utumishi.
Imeeleza kwamba, Rais mara baada ya kufanya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu wakiwemo, mawaziri, manaibu waziri, jaji mkuu na naibu jaji mkuu, viongozi hao watalazimika kuthibitishwa na Bunge.

No comments:

Post a Comment