Idhaa ya kiswahili ya UMOJA MATAIFA (UM). Asubuhi ya leo inasema ... Wakati jana dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ajira kwa watoto, Rais Joyce Banda wa Malawi amezungumza katika mkutano wa kimataifa wa shirika la kazi duniani, ILO na kusema nchi yake itachochea harakati za kupiga vita vitendo hivyo dhalimu kwa watoto vinavyowanyima haki zao za msingi ikiwemo kwenda shule.
Hotuba ya Rais Banda imeenda sambamba na siku ya kimataifa ya kutokomeza ajira kwa watoto ikimulika zaidi, ajira za majumbani.
Rais Banda amewaeleza washiriki wa mkutano huo mjiniGeneva, Uswisi ya kwamba yeye binafsi anasikitishwasanana ajira za watoto hususan kwenye nchi zinazoendelea ikiwemoMalawi, akitaja chanzo kuwa ni umaskini.
Amesema familia maskini zisizo na ajira zenye hadhi zinajikuta watoto wao wakitumbukia kwenye ajira za utotoni.
Amesema ukuaji wa uchumi wa Malawikwa asilimia sita kati ya mwaka 2004 na 2009, haukuweza kuepusha watoto na ajira kwa kuwa haukutoa fursa za ajira za kutosha.
"
KAULI YA BI JOYCE BANDA
"Naahidi kuendelea na
harakati za kutokomeza ajira kwa watoto nchini Malawi, na pia kuimarisha
mipango ya kutokomeza umaskini ambao ni chanzo kikuu cha tatizo hilo.Nategemea
ILO kama shirika la kufanya nalo kazi kwenye suala hili."
ILO inasema zaidi ya watoto Milioni Kumi na
Nusu wengine wakiwa hata na umri wa miaka mitano wanahusishwa na ajira za
majumbani, na wengi wao ni watoto wa kike.
No comments:
Post a Comment