Monday, June 10, 2013

STARS WAMELINDA HESHIMA1 BIG UP






Taifa Stars imelala kiume kwa Morocco kwa kukubali kipigo cha bao 2-1 toka kwa wenyeji Morocco. Taifa Stars pamoja na kufungwa ilionyesha kiwango cha soka cha hali ya juu ingawa ilicheza kwa muda mrefu ikiwa pungufu baada ya Agrey Morris kupewa kadi nyekundu kwenye dakika ya 37. 

Ikicheza pungufu kwa muda mrefu wa dakika zaidi ya 55, Taifa Stars ilionyesha kiwango kizuri sana cha mchezo pamoja na kuwa pungufu.

Taifa Stars ilifanikiwa kupata goli lake la kufutia machozi kwenye dakika ya 61 kupitia kwa Amri Kiemba ambaye aliachia shuti kali lililoenda moja kwa moja nyavuni na kumuacha golikipa wa Morocco akigaragara.

Morocco ilipata bao lake la ushindi kwenye dakika ya 51 baada ya mshambuliaji wa Morocco, El Arabi kubaki peke yake na kipa wa Stars Juma Kaseja, alimpiga chenga Kaseja na kuuzamisha kwenye nyavu za kati za Stars.

Refa aliishaiharibu mechi kwa kutoa kadi nyekundu ambayo haikuwa halali kwa kwa Aggrey Morris kwenye dakika ya 37.

Morocco ilipata goli la kuongoza kwa penalti kwenye dakika ya 37 baada ya beki wa Taifa Stars Agrrey Morris kujikwaa na kumuangukia mshambuliaji wa Morocco ambaye alikuwa tayari offside kwenye eneo la penalti. Morris amepewa kadi nyekundu.

Washambuliaji wawili wa Morocco walikuwa tayari offside lakini refa alipeta na Morris alipojikwaa wakati akajaribu kuokoa refa amempa kadi nyekundu kwa kumwangusha mshambuliaji wa Morocco.
 
Kikosi cha Taifa Stars kilichoshuka dimbani NI: JumaKaseja (c); Kapombe, Nyoni, Yondan, Morris; Domayo, Sureboy, Kiemba; Ngassa, Samatta & Ulimwengu

No comments:

Post a Comment