Wakati Serikali,
mashirika ya kidini na asasi za kiraia ya zikikemea ukatili wa kijinsia, imebainika
kuwa wafanyakazi wa wakiume wa majumbani hutumia sehemu zao za siri
kuwanyonyesha watoto wachanga pindi wanapo lia wakati wazazi wao wakiwa kwenye
majukumu ya kazi.
Hayo yamebainika
kwenye semina ya wanawake iliyoandaliwa na asasi ya kiraia ya Tree of Hope
iliyopo jijini Tanga yenye lengo ya kutathimini vitendo vya ukatili vinavyo
endelea mkoani hapa na jinsi ya kutafuta ufumbuzi wa kukomesha vitendo hivyo
vyenye viashiria vya ukatili, unyanyasaji kijinsia nakuto thaminiwa kwa utu wa
mwanamke.
TERESIA KAPINGA anaelezea
kwa uchungu jinsi wafanyakazi wandani wanavyowafanyia ukatili watoto wachanga
kwa kuwanyonyesha sehemu zao za siri.
Aidha MWANSHAMBA
MWANDAU na EVA MBWANA wameiomba serikali kuchukulia hatua kali za kisheria watu
wanaojihusisha na biashara ya kuuza mabinti kwa wanaume, ambapo wanafunzi wa
kike wamewaomba wajumbe wa baraza la katiba wilaya kuingiza maoni ya
kuharalisha utoaji wa mimba katika rasimu ya katiba mpya ambazo
wanazopata pindi wakiwa masomoni zitokanazo na kubakwa au kwa kufanyiwa
ukatili pasipo ridha yao.
Mkuu wa Mkoa wa
Tanga mh. CHIKU GALAWA amesema kwa mujibu wa tafiti za mwaka 2010
zinaonyesha ukatili wa kimwili unaongoza, ukifuatiliwa na ukatili wa kingono
ambapo ukatili kwa wajawazito umechukua nafasi ya tatu mkoni Tanga.
MKUU WA MKOA WA TANGA mh. CHIKU GALAWA
= = = = =
No comments:
Post a Comment