MATONYA
SONGEA
Msanii huyo amekamatwa
kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa
Jambolee uliopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Baada ya kuja ukumbini
akiwa amelewa hali iliyomlazimu kushindwa kufanya show na kusababisha hasara
katika ukumbi baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbini hapo, Ndipo
waandaaji wa show hiyo walipo amua ifanyike siku iliyofuatia na
kiingilo kiwe ni kununua bia tu .
Wakati huo msanii huyo
alitakiwa akafanye show nyingine wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya
mkataba wao lakini hakufanya hivyo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi
kurejea kwake, Dar es Salaam , Baada ya kuvuja taarifa hizo walimfuata
hadi alipofikia nakukuta amehamia sehemu nyingine.
Waandaji hao waliamua
kuchukua hatua ya kumvizia katika Bus ndipo alipokamatwa , Hadi sasa yupo
mahakama ya mwanzo , Taarifa zaidi tutawaletea
via/ demashonews blog
No comments:
Post a Comment