Katibu
Mkuu wa Zamani Ofisi ya Rais Ikulu,Mzee Timothy Apiyo (pichani), amefariki
dunia katika hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini alikokuwa amelazwa.
Marehemu
Mzee Apiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Ikulu kwa Kipindi kirefu mpaka alipostaafu na
kuhamia Kinyerezi jijini Dar es Salaam. Anatajwa kuwa ni mmoja wa viongozi
waandamizi waliokuwa hawana masihara kazini, kiasi hata viongozi serikalini
walikuwa wakimheshimu sana.
Mipango
ya kuusafirisha mwili wa marehemu Mzee Apiyo inaendelea nasi tutawafahamisha
kila hatua kwa kadri tutavyopata ripoti hizo.
Timothy
Apiyo, alizaliwa katika wilaya ya Rorya, Tarafa ya Suba, mkoa wa Mara. Alipata
elimu ya msingi na sekondari akiwa hapo na mwaka 1959 alijiunga na Chuo Kikuu
cha East Afrika na kuchukua digrii ya kilimo.
Baada
ya kuhitimu aliingia serikalini wakati huo Tanzania ikiitwa Tanganyika, na
baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda. Mwaka 1959
alihitumu Makerere na kupangiwa kufanya kazi katika Chuo cha Kilimo cha
Ukiliguru.
Mwaka
1960 alihamishiwa wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga kuwa Bwana Shamba wa Wilaya na
mwishoni mwa mwaka huo akahamishwa tena kwenda Wilaya ya Ifakara mkoani
Morogoro ambako alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha
Ilonga.
Alikaa
Ilonga hadi Agosti 1962 ambapo alipata ufadhili wa kwenda kusoma Marekani
katika Chuo Kikuu cha West Virginia ambako alichukuwa digrii ya pili ya Sayansi
ya Kilimo na kutunukiwa cheti mwaka 1963.
Baada
ya kurejea nchini, mwaka 1964 alipangiwa kufanya kazi Wizara ya Kilimo na
baadaye akapelekwa Shinyanga kuwa Ofisa Kilimo wa Mkoa. Desemba 1965
alihamishiwa mkoa wa West Lake (Sasa Bukoba). Na mwakan 1967 akarudishwa
wizarani nikiwa Afisa Mipango Mwandamizi.
Mwaka
1968 akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango Kilimo katika Wizara ya Kilimo na
mwaka uliofuata 1969, akawa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Nyumba, Ardhi na
Maendeleo Mijini. Novemba 1969 alirudishwa tena Wizara ya Kilimo kuwa Katibu
Mkuu na Aprili 1972 akapata uhamisho kwenda kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Biashara
na Viwanda.
Aprili
1974 Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Julai 1986
alistaafu kazi
No comments:
Post a Comment