.Shindano
la kumtafuta mrembo wa dunia kwa mwaka huu 2013 linategemewa kufanyika huko
Indonesia, lakini utofauti utakaokuwepo ni kwamba washiriki hawatavaa vazi la
bikini kama ilivyozoeleka katika mashindano yaliyopita.
Kwa
mujibu wa mtandao wa aceshowbiz waandaaji wa shindano hilo la mrembo wa dunia
2013 wametoa taarifa ya uamuzi huo Jumanne wiki hii (June 5) ikiwa ni hatua ya
kuepukana na kutofautiana na vikundi vya kiislam vya Indonesia ambayo aslilimia
90 ya wananchi wake ni waislam.
Msemaji
wa RCTI waandaaji rasmi wa Miss World 2013 nchini Indonesia, Adjie S.
Soeratmadjie alisema“Kutakuwa hakuna bikini katika shindano la miss world mwaka
huu ili kuheshimu mila zetu za jadi na maadili, Hili ni suala nyeti hapa Indonesia..
Tumejadiliana tangu mwaka jana na wamekubali.”
Shindano
hilo linatarajiwa kufanyika mwezi september mwaka huu (2013).
No comments:
Post a Comment