Wandishi wa Habari Mkoani Mbeya
wametakiwa kuisaidia jamii kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na
Watoto uliokithiri vitendo ambvyo hupelekea kuwa na ongezeko la maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi.
Mwezeshaji kutoka Walter Reed
Program Hijja Wazee wakati akitoa Semina kwa waandishi wa Habari 20
iliyofanyika katika ukumbi wa Youth Centre wa Kanisa Katoliki uliopo Jijini
Mbeya.
Hongera mpiga picha nimependa picha ilivyotokelezea!
Mwezeshaji kutoka Walter Reed
Program Mergitu Ebba akiwanoa waandishi wahabari waliohudhuria semina hiyo.
Mergitu Ebba, ndo hivyo!
Baadhi ya waandishi wakifuatilia
mada
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu Blog
akifuatilia mada na ndiye aliye iwezesha KEGAJO KUPATA MZIGO HUU
Nukuu muhimu.
Baba kaenda kazini
Gender ilizingatiwa
Hijja Wazee akitoa mada
Wawezeshaji wakisikiliza kwa makini wadau wao
Wandishi wa Habari
Mkoani Mbeya wametakiwa kuisaidia jamii kupinga vitendo vya unyanyasaji wa
kijinsia na Watoto uliokithiri vitendo ambvyo hupelekea kuwa na ongezeko
la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Kauli hiyo
imetolewa na Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Hijja Wazee wakati akitoa
Semina kwa waandishi wa Habari 20 iliyofanyika katika ukumbi wa Youth Centre wa
Kanisa Katoliki uliopo Jijini Mbeya.
Mkufunzi huyo
amesema kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa Kijinsia ndani ya jamii
vinaweza kumalizwa endapo Wanahabari watafanya kazi ya kujitolea ya kuibua na
kuiambia jamii madhara ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa
zaidi ya asilimia 60 ya jamii ya Mbeya inasadikika kujihusisha na vitendo vya
ukatili wa kijinsia na kwamba Mfuko wa raisi wa Marekani umetoa fedha kwa ajili
ya kuhakikisha Vitendo hivyo vinaisha ambapo msaada huo utalenga Nchi tatu
ikiwemo Tanzania.
Amesema Nchini
Tanzania ni Mikoa minne itakayohusika ambayo ni Mbeya, Iringa, Mara
na Dar Es Salaam ambapo kwa Mkoa wa Mbeya ni Wilaya Sita zitakazohusika ambazo
ni Mbeya Jiji, Ileje, Kyela, Rungwe, Busokelo na Mbeya Vijijini.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment