Monday, June 3, 2013

SUBRA YAVUTA KHERI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Kamati ya msiba wa Albert Mangwea walitoa  taarifa kwamba mwili wa   Albert Mangwea hautoweza kufika siku ya jana  jumapili ya tarehe 2/06/2013 kama ilivyo taarifa hapo awali, hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao.
Kwa sasa tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wenzetu/wawakilishi wetu waliopo nchini Afrika Kusini, mara tutakapopata taarifa hizo tutawafahamisha zaidi.
Tunaomba radhi watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza tushirikiane na uvumilivu kwa hili.
Asante
Mwenyekiti wa Kamati
Kenneth Mangweha


No comments:

Post a Comment