Mzee Nelson Mandela
Madaktari wanaomtibu rais wa zamani wa
Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa
ishirini na nne zilizopita na sasa ni mahututi.
Habari hizo zimekuja kupitia taarifa
iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.Taarifa hiyo imesema bado Mzee
Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita
akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma
amemtembelea Mzee Mandela jana jumapili jioni na kuzungumza na jopo la matatibu
wanaomtibia.
Baadaye bwana Zuma alirejea kauli yake ya
kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela apate nafuu.
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment