Mechi hiyo kali ya La Liga imechezwa katika Uwanja wa
Santiago Bernabéu, Madrid nchini Hispania.
MSHAMBULIAJI mahiri wa
Barcelona, Lionel Messi, amepeleka vilio kwa mashabiki na wapenzi wa
Real Madrid baada ya kufunga 'hat-trick' wakati timu yake ikishinda bao 4-3
dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.
Mshambuliaji huyo amefunga mabao mawili kwa penalti
dakika ya 65 na 84 wakati lingine akilifunga dakika ya 42 baada ya Andres
Iniesta kufunga mapema dakika ya 7
Mabao ya Madrid
yamewekwa kimiani na Karim Benzema aliyetupia mawili dakika ya 20 na 24 la tatu
likifungwa na Mchezaji Bora wa Dunia mwaka 2013/14, Cristiano Ronaldo kwa
mkwaju wa penalti dakika ya 55.
No comments:
Post a Comment