Monday, April 30, 2012

Jicho Limekubalije?

Kiukweli kabisa! si kila mtu anayeiweza hii sanaa ya jicho! kuchonga nyusi iendane na jicho la mhusika! si wote! wengi  huwa wanaharibu muonekano wa jicho la mtu!

kutoka ndani ya nafsi yangu ningetamani mi kuwa na uwezo wa kumchonga mtu nyusi akapendeza kama huyu ,ingawa huwa nawachonga baadhi ya watu ambao huwa wanaamini nawapatia! lol

kope sasa! hilo jicho hapo juu limekubalije? hapo limefumbwa! likiinuliwa weee! utadhani anakwita kumbe anakutazama tu. eye shadow imekubali na kope zimebandikwa vizuri mnppp! hapo ndo nnapotamani kubandika ila nikifikiria gundi! mh naishiwa nguvu! big up kwa wale wanawapatia watu kuwapaka eye shadow ,kubandika kopa na kuchonga nyusi! ambao bado si vibaya kujifunza na kufanya vizuri zaidi!
jumatatu njema.

Make Up Za Sasa?

 
Mi huwa napenda sana urembo ila ukizidi sana huwa naona hata aibu kumuangalia mtu usoni.lakini naamini kua si make up zote za uso na macho zinawafaa watu wa rangi zote!tazama make up hii ni kwa mtu mweupe ukimpaka mweuzi inakuaje?

Urembo Wa Kope

habari za jumatatu ya leo! kila uchao jinsi ya kike inajaribu kupata vitu vya kuukana uzee na kuuamsha uso ili tu kuonekana na jinsi me! ingawa urembo wa sasa si wazamani wa mama zetu kuweka majaribosi masikioni kisha baasi imekwisha! lah hasha siku zetu tunaikosoa kazi ya Mwenyezi kwa kuongeza vitu!

nianze na jicho! wanasema mwana mke reception babu! lakini kiukweli jinsi reception hiyo inavyo andaliwa ili kua na mvuto! wakati mwingine huleta madhara! mfano ni hizi kope za kuongeza!
1- aliyeweka kope sharti la kwanza asiziondoe mwenyewe!
2- nina wasiwasi na gundi itumikayo kwani rafiki yangu aliweka kiasi cha kunitamanisha nami nitake kuweka nikasita kutokana na rafiki yangu kuwashwa sana macho ,yakaanza kujaa maji, kuvimba na hatimaye kutoka usaa kopeni! alikuja kuponea hospitali!

sasa enyi muwekao kope ni kwa faida ya nani na huku maumivu kwa baadhi yenu ni dhahiri!?  mwisho aloweka kope kulia kwake awapo msibani ni kwa mashaka akilinda kope zake zisinyofoke! lol niwieni radhi urembo wenye madhara na masharti mi siuwezi waungwana. kesho naja na midomo. jumatatu njema yenyee kijimvua mvua.

siku njema...

Tuesday, April 24, 2012

Kim Kardashian ashirikisha nini apakacho ili kuleta muonekano wa ngozi yake

Na hii ni baada ya kila anapotokea kwenye jamii, watu humuuliza anapaka nini kwenye ngozi yake mbona ana mvuto? Akaona isiwe taabu akatupia nini kinacho mfanya awake wake.
Ki ukweli usiwe mchoyo kushare na wenzio kinachokufanya uwe na mvuto! Na akaamua kutupia picha hizo katika ukurasa wake wa twitter, kwa kifupi Kim anaonekana kama na kitu cha manjano ambayo sisi bongo tunayo ama unga wa dengu hivi. angalia
Picha ya juu ni baada ya kutoa kile alichokipaka hakuna maajabu hata wewe waweza ng’arisha ngozi yako kwa vitu vya asili
Katika ukurasa wake wa twitter akatupia kichwa cha habari hiki She bila kuongeza ama kupunguza neno 'Glamming up with @1maryphillips!!!  Matokeo mazuri ya kile anachojipaka yamemchanganya Kim mwenyewe ila anajua kitamtengeneza
Kim hakusita kumuweka hadharani Mtu ambaye amempa mchanganyo huo na kwamba ni mtaalamu wa masuala la make up au make up artist anaitwa Mary Phillips, na amesababisha masuper star kama  Jessica Simpson, Jennifer Lopez na Salma Hayek  na kueleza kua ni miongoni mwa wateja wao
Kim  pia baadae alionesha picha ya matokeo ya alichokipaka na kuandika mngao kiasi na hii ndio picha yenyewe .
Mpira ukiwa umedhitiwa: Kim baada ya kung’arisha ngozi yake na kujipodoa alishiriki  katika Jeep na sherehe  za USA Basketball  .
Nguo ina rangi ijulikanayo kama Mellow yellow: Kim akionesha umbo lake katika nguo inayoonesha vilivyo umbo lenye mvuto na viatu vyenye kumkamata
Umbo  la kifua lenye mvuto la Kim
Kim mwenyewe anaeleza kua make up inafurahisha lakini pia ni moja ya mapambo ya mwanamke  ingawa mara kadhaa ameshatoka na kupigwa picha akiwa hajapaka make up na anasema kitendo cha kutopaka make up na kusimama mbele za watu kina mpa nguvu na haona aibu kuwaonesha watu jinsi alivyo na ana furahia jinsi alivyo
Hata kama ni burudani kupaka make up kitu kikubwa cha msingi ni kuikubali ngozi yako ukiwa na make up ama ukiwa hujapaka make up!
Mpo? Neno hilo, wale  ambao huwezi toka bila make up kubalini ngozi zenuuu!!!!!!
CIOA

Wivu wa Mapenzi Amuunguza Kwa Pasi ya Moto Mkewe

NewsImages/6373006.jpg
Mke wa Henry baada ya kuunguzwa vibaya na moto wa pasi
Mwanaume mmoja wa nchini Nigeria anashikiliwa na polisi kwa kumuunguza na pasi ya moto mkewe sehemu mbali mbali za mwili wake zikiwemo sehemu zake za siri kwa kile kilichodaiwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na baba yake mzazi.
 
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Henry Nnamdi mkazi wa jiji la Lagos nchini Nigeria, alimuua mtoto wake mchanga kwa kukibamiza kichwa chake kwenye sakafu mpaka alipofariki.

Henry hakuishia hapo alimchukua mke wake wa ndoa yao ya miaka miwili na kumfunga na kamba kwenye kiti kabla ya kutumia pasi ya moto kumuunguza mkewe sehemu mbali mbali za mwili wake.

Henry alimuunguza vibaya mkewe kwenye matiti yake na sehemu zake za siri na sehemu mbali mbali za mwili wake kiasi cha kumfanya mkewe apoteze fahamu na hajazinduka hadi sasa.

Chanzo cha yote ni wivu wa Henry kuwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na baba yake Henry na kwamba huyo mtoto wake mchanga si mtoto wa damu yake kibailojia.
Henry anamtuhumu baba yake mzazi kutembea na mkewe.

Tukio hilo lililoutikisa mji wa Lagos, lilitokea wakati wa sherehe za pasaka mwezi huu ambapo majirani wa kitongoji cha Okota walishtushwa usiku usingizini na kelele za kuomba msaaada za mke wa Henry aliyejulikana kwa jina moja la Nnamdi.

Mke wa Henry huku akilia kwa uchungu wa maumivu ya kuunguzwa na moto wa pasi, aliwaita majirani waje kumuokoa.

Baada ya majirani kusita sita kuingia ndani ya nyumba ya Henry, walilazimika kuvunja mlango na kuingia ndani baada ya kelele za maumivu za mke wa Henry kuzidi.

Waliyoyashuhudia ndani baadhi walishindwa kuyangaalia kwa mara ya pili waligeuza njia na kurudi walikotoka na kwenda kuwaita polisi.

Polisi waliwahi kufika na kumkuta mke wa Henry akiwa amezimia hajitambui na maiti ya mtoto wake mchanga ikiwa kwenye sakafu.

Henry alikamatwa na kutiwa mbaroni huku mkewe akiwahishwa hospitali ambako madaktari hadi sasa wanapigania maisha yake ingawa bado fahamu zake hazijamrudia.