Thursday, May 24, 2012

Hisa za Facebook zazua utata


Morgan Stanley

kwa wale wapenzi wa mtandao wa kijamii wa Face book hii inakuhusu! Kumetokea utata mpya kuhusu hisa za Facebook katika masoko ya hisa wiki iliyopita baada ya wasiwasi kuzuka kutokana na mauzo ya hisa hizo wiki iliyopita na jinsi zilizouzwa.
Wasimamizi wa fedha wanachunguza iwapo kiongozi wa mpango Morgan Stanley, aliwadokeza baadhi tu ya wateja wake kuwa faida ya hisa za Facebook zilizotarajiwa zimeshushwa daraja.
Morgan Stanley amekanusha hilo na kusema kuwa uuzaji wa hisa hizo ulifuata kanuni sahihi.Bei za hisa za kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii imeshuka tangu mauzo yake kuzinduliwa rasmi kwa umma Ijumaa iliyopita.
Matatizo ya kiufundi katika siku ya kwanza ya mauzo hayo yalisababisha baadhi ya wawekezaji kupoteza fedha.

Daktari wa Osama afungwa jela








                                                        Osama Bin Laden

Maafisa wa serikali ya Pakistan wamesema kuwa aliyekuwa daktari wa Osama Bin Laden amehukumiwa miaka thelathini Gerezani.
Daktari huyo alituhumiwa kuwasaidia maafisa wa ujasusi wa Marekani CIA kumsaka Osama Bin Laden na atahudumia kifungo chake nchini Pakistan.Ripoti zinasema kuwa Shakil Afridi alipatikana na hatia ya uhaini.




Shakil Afrid

Afridi anatuhumiwa kuendesha mradi bandia wa kutoa chanjo ambao unaaminika kusaidia maafisa wa CIA kumnasa Osama bin Laden katika maficho yake mjini Abottabad, ambako aliuawa na wanajeshi wa kitengo maalum cha marekani mwezi mei mwaka uliopita.
Waziri wa mambo ya nje wa marekani Bi Hillary Clinton, ametoa wito kwa serikali ya Pakistan  kuachiliwa kwa bwana Afridi, akisema kuwa kazi yake imekuwa na manufaa kwa serikali za Marekani na Pakistan.


Hillary Clinton

waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton anajaribu kutumia Diplomasia ili shakil aachiliwe huru kwani manufaa wameyapata Pakistan,Marekani na pengine dunia kwa ujumla.

Nzi zaidi ya wawili wasipige kelele China








Serikali ya China imetangaza kuwa choo chochote cha umma hakitakiwi kuwa na nzi zaidi ya wawili wanaoruka kwa wakati wowote.
Hiyo ni moja kati ya mfululizo wa viwango vipya vilivyowekwa na mamlaka hiyo kujaribu kuyafanya bora maeneo ya umma mjini humo.Malengo mengine yanahusu usafi, matumizi ya vifaa na mafunzo kwa watendaji.
Mwandishi wa BBC aliyeko Beijing anasema sheria hizo mpya zimelenga watu wanaoishi katika maeneo ya zamani ya mji huo.

Wednesday, May 23, 2012

Mwanaume Mwenye Watoto 30 Kwa Wanawake 11


Desmond Hatchet

mwanamume huyo hapo juu ana umri wa miaka 33, ana  watoto 30, na wanawake 11, naamini wakati anakula tunda alikua hafikirii kwa makini juu ya gharama za maisha! au pengine kutokana na utaratibu wa nchi yake ya Marekani anaweza akasaidiwa kulea watoto akitoa ombi, labda ndo maana akatekeleza kimoja kati ya vifungu vya  maandiko kua zaeni mkaongezeke! labda! sina hakika.

Desmond alijipatia umaarufu duniani mnamo mwaka  2009 wakati huo alikua na watoto wapatao 21,miaka mitatu baadae akaongeza watoto 9 na kufanya idadi ya watoto wake kufikia 30. Na yeye mwenyewe anatoa ushuhuda bila soni kua “kwa miaka 2 iliyopita nilipata watoto 4,wastani wa watoto 2 kwa mwaka.alikua anaona utaaaamu!

Lakini sasa! Gharama za malezi kwa watoto wake zinampa stress kiasi cha kumfanya ahahe kuomba msaada wa matunzo,akaanzia mahakamani kuomba imuonee huruma isi chop his money kutoka katika salary yake.kisa  nusu ya mapato yake yote anayoyapata kwenye kazi yake huenda wa mama wa watoto wake, kipato chake ni kidogo hivyo dunia naiona chungu.

Sasa basi Desmond ameiomba mahakama mjini Tennessee imtafutie njia za kumuwezesha yeye kumudu gharama za malezi ya watoto wake.
Kati ya watoto hao 30,mtoto wake mkubwa kuliko wote ana umri wa miaka 14 tu! Chezea weye! Tafakari kabla ya kutenda!



full stress babake,sorry, but am glade umeomba msaada! lets hope watasikia kilio chako

Didier Drogba kuondoka Chelsea





Mshambuliaji Didier Drogba ataihama timu ya Chelsea ya England msimu huu wa joto, baada ya kuichezea  klabu hiyo  kwa muda wa miaka 8. Mchezaji huyo wa Ivory Coast, mwenye umri wa miaka 34, alifunga bao la ushindi katika fainali ya mwaka huu ya Kombe la klabu Bingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern.
Drogba atakuwa huru kujiunga na klabu yoyote ile, kwani mkataba wake na timu ya Blues unaelekea kwisha. Baada ya miezi mingi ya mashabiki kutojua hatma yake, Drogba amethibitisha sasa ataondoka Stamford Bridge.
"Nilitaka kukomesha hali hii ya shaka na kuthibitisha kwamba ninaondoka Chelsea", alielezea Drogba katika tovuti ya Chelsea."Umekuwa ni uamuzi mgumu sana kwangu, lakini ni fahari kwangu kwa ufanisi tulioweza kupata, lakini wakati umewadia kwa changamoto mpya",.Aliongezea: "Kama timu, tumefanikiwa katika mengi, na tukashinda vikombe muhimu."
"Ningelipenda kuitumia nafasi hii kuwashukuru wote katika klabu, hasa Roman Abramovich na wachezaji wenzangu."Tatizo la mkataba wa Drogba ulianza msimu uliopita, wakati klabu kilipokataa kumuongezea miaka miwili zaidi katika mkataba wake.
Wasiwasi wa mashabiki ulizidi wiki chache zilizopita, iwapo Drogba ataendelea kuichezea Chelsea, hasa baada ya timu yake kuibuka mshindi katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Liverpool, na pia alipofunga bao la kusawazisha Jumamosi, na vilevile kufunga goli la ushindi wakati wa mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Bayern

Akutwa na hatia ya kumuua Terrebblance


Patrick Ndlovu na Chris Mahlangu


Mmoja kati ya wanaume wawili walioshtakiwa kwa kumuua Eugene Terreblanche mwaka 2010 amepatikana na hatia.Chris Mahlangu, alipatikana na hatia ya mauaji ingawa mshtakiwa mwenzake Patrick Ndlovu, aliachiliwa kwani alikuwa na miaka kumi na tanao wakati wa kitendo hicho.
Polisi waliimarisha doria katika mji wa Ventersdorp, nchini Afrika Kusini wakati hukumu ikisubiriwa kwa vijana hao wawili wa Kiafrika waliotuhumiwa kumuua Eugene Terre' Blanche miaka miwili iliyopita
Bwana Terre' blance alikuwa kiongozi wa mrengo wa kulia wa vuguvugu la kupigania utawala wa kizungu la Afrikaan Resistance Movement




                                                                Terre' Blance


Wanaharakati wengi wa kutoka vuguvugu walipiga kambi nje ya mahakama hiyo wakiwa wamevalia sare za chama hicho na wamebeba bunduki.Wawili hao walikanusha mashtaka ya kumuua muajiri wao na kutekeleza uwizi wa mabavu.
Mahlangu anadai kuwa alikuwa akijitetea ili hali mvulana anayeshtakiwa pamoja naye amekanusha kuhusika na uhalifu huo.Kizingiti kikubwa katika kesi hii ni kuwa Mahlangu na mvulana huyo walikataa kutoa ushahidi wao, wakati wa kesi hiyo.Hali ya wasi wasi ilitanda nje ya makahakama hiyo kama ilivyokuwa wakati wa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo miaka miwili iliyopita.
Wakati huo, polisi walikabiliwa na wakati mgumu kuwatenganisha makundi ya wafuasi wa pande hizo mbili.Lakini idara ya polisi na chama cha AWB zimesema kuwa ghasia zozote hazitarajiwi.
Polisi wamesema ikiwa mambo yatakwenda kinyume na matarajio yao, imeweka mikakati thabiti ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote atakayevuruga shughuli za mahakama.
Mwezi uliopita, wakati mawakili walipokuwa wakitoa tetesi zao za mwisho mbele ya mahakama hiyo, jaj I alionya kuwa hukumu huenda ikachukua muda mrefu lakini haijulikani, ikiwa uamuzi huo utachukua zaidi ya siku moja kutolewa.
Hata hivyo pande zote zinatarajiwa kukata rufaa baada ya hukumu kutolewa.


FIFA yachagua mwanamke


Lydia Nsekera


Shirikisho la soka duniani limemteua mwanamke wa kwanza kwa kamati yake kuu.
Lydia Nsekera ni rais wa shirikisho la soka la Burundi kwa sasa na atashikilia wadhifa huo mpya katika fifa kwa mwaka mmoja ujao hadi uchaguzi rasmi mwaka 2013.
Kama moja ya kuangamiza ufisadi shirika hilo limemteua mwanaviwanda mmoja kutoka uswizi Domenico Scala kusimia kamati mpya ya uhasibu kusimamia matumizi yake ya mwaka.


                                                                          Domenico Scala